Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando, mke wake Eva Mhando, walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka sita ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka, kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Mhando alikuwa anatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka kwa kuipa zabuni Kampuni ya Santa Clara Supplies Ltd huku akijua ana maslahi nayo na kwamba anaimiliki yeye, mke na watoto wake.
April 14 2016 Mahakama ya Hakimu mkazi kisutu Dar es salaam imemuachia huru baada ya kuona hana hatia kwa kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibisha juu ya matumizi mabaya ya ofisi na ughushaji wa nyaraka ambao inadaiwa na maafisa wa serikali kuwa kampuni hiyo ilifanya hivyo ili kupewa zabuni ambayo ilitaka kupewa na bodi hiyo ya Tanesco
Mahakama imesema Mhando alikuwa haingii kwenye vikao vya maamuzi ya bodi ya Tanesco kwa hiyo alikuwa hana ushawishi wa moja kwa moja kushawishi kwamba kampuni hii ya Santa Clara ambayo ni ya mke wake kwamba ipatiwe zabuni.
No comments:
Post a Comment