Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (Mb) amekutana
na Waziri wa Habari na Mawasiliano wa nchi ya Vietnam Bwana Nguyen Bac
Son ofisini kwake kwa lengo la kupanua wigo wa uwekezaji kwenye Sekta ya
Mawasiliano nchini Tanzania na kushirikiana kwa pamoja kuendeleza Sekta
hizo baina ya Tanzania na Vietnman. Kikao hicho ni muendelezo wa ziara
ya Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang na
ujumbe wake nchini Tanzania.
Prof.
Mbarawa alisema kuwa Tanzania imekuwa na ushirikiano na Vietnam kupitia
Kampuni ya Viettel kwa kuwekeza kwenye miundombinu ya kufikisha huduma
za mawasiliano vijiini kwa kutiliana saini Mkataba.
Mkataba
huo ni wa miaka mitatu kuanzia mwezi Oktoba mwaka 2014 hadi Novemba,
2017 ikijumuisha ujenzi wa miundombinu ya Mkongo wenye urefu wa kilomita
20,000 kwenye wilaya zote nchini; kujenga miundombinu ya mawasiliano
kwenye vijiji 4,000; kuunganisha Ofisi za Wakuu wa Wilaya; hospitali za
Wilaya; Ofisi zote za Posta za Wilaya; na kupeleka na kutoa huduma za
intaneti bila malipo kwenye shule 3 za Sekondari za Serikali katika kila
Wilaya nchini kwa kipindi cha miaka mitatu.
Aidha,
Prof. Mbarawa aliongeza kuwa tangu Kampuni ya Viettel yenye jina la
biashara la Halotel ilipoanza kufanya kazi rasmi mwezi Oktoba mwaka
2015, imeweza kupeleka huduma ya mawasiliano maeneo ya vijijini na hadi
hivi sasa ina watumiaji wa simu za mkononi wapatao milioni 1.2 na
wananchi walio wengi wanafurahia huduma hiyo tofauti na hali ilivyo kuwa
hapo awali kipindi cha miezi sita iliyopita na ikizingatiwa kuwa sehemu
nyingine za vijijini hapakuwa na mawasiliano. Pia alisema kuwa,
“Serikali
ya Tanzania itaendelea kujenga na kuwekeza kwenye Sekta ya Mawasiliano
ili kuwavutia wawekezaji na kampuni za simu za mkononi ambapo Serikali
ya Tanzania ilitoa ruzuku kiasi cha dola za marekani milioni 30 ili
kuziwezesha kampuni hizo kupeleka mawasiliano vijijini na maeneo
yasiyokuwa na mvuto wa kibiashara”.
Hadi
kufikia mwezi Machi, 2016 Halotel imejenga Mkongo wenye urefu wa
kilomita 18,000 kati ya kilimota 20,000; na kujenga miundombinu ya
mawasiliano kwenye vijijini 1,605 kati ya vijiji 4,000 visivyokuwa na
mawasiliano.
Katika
mazungumzo hayo ya kuendeleza sekta ya Mawasiliano Tanzania, Prof.
Mbarawa aliwaalika wawekezaji kutoka Vietnam wa Sekta ya Mawasiliano na
kampuni ya Halotel kujiandaa na kuja Tanzania kushiriki mnada wa kununua
masafa ya 700MHz ambayo yamepatikana baada ya kuhama kutoka Teknolojia
ya Utangazaji ya Analojia na kuhamia Teknolojia ya Utangazaji ya
Dijitali.
Pia
alisema kuwa Kampuni za Vietnam zinakaribishwa kuanzisha na kuendeleza
huduma za mawasiliano za mfumo wa kumpatia mteja huduma tatu kwa pamoja
ya sauti; intaneti; na kuangalia televisheni ikijulikana kwa jina la
triple player ili Tanzania iweze kwenda sambamba na kasi ya ukuaji wan a
maendeleo ya TEHAMA yanayotokea dunia nzima.
Katika
kikao hicho, Prof. Mbarawa alimweleza Mhe. Ngoyen Bac Son kuwa Tanzania
iko tayari kusaini Mkataba wa Makubaliano ya ushirikiano na Serikali ya
Vietnam wa kubadilishana wataalamu kwenye Sekta ya Mawasiliano na
kuwapatia mafunzo ili kujenga uwezo wa wataalamu wetu wa Tanzania; na
kuanzisha na kuendeleza viwanda vidogo vidogo vya TEHAMA (ICT Small
Scale Factories) nchini Tanzania ambapo viwanda hivyo vitazalisha ajira;
kurahisisha upatikanaji wa vifaa na huduma za TEHAMA kuendana na
mahitaji na mazingira yetu; kuongeza mapato; na kuwahudumia wateja wa
nchi za jirani na Tanzania.
Mhe.
Ngoyen Bac Son alisema kuwa Serikali ya Vietnam iko tayari kuendeleza
ushirikiano baina ya Serikali yao na ya Tanzania ya kuendeleza Sekta ya
Mawasiliano; na sekta ya kukuza Uchumi na Maendeleo ya Tanzania kama
alivyozungumza Rais wa Vietnam. Pia aliongeza kuwa,
“Serikali
ya Vietnam iko tayari kuleta kampuni za kuwekeza Tanzania kwa kuanzisha
Kiwanda cha vifaa vya mawasiliano kwa ajili ya kuwapatia watanzania
huduma za mawasliano na ni matarajio yetu kuhakikisha kuwa ni kiwanda
kikubwa ambacho kitahudumia na wateja wa nchi za jirani na Tanzania”.
Aidha,
Mhe. Ngoyen Bac Son aliongeza kuwa Serikali ya Vietnam inaridhia
kusaini Mktaba wa Ushirikiano baina ya nchi hizo na amewakaribisha
wafanyabiashara na kampuni za Tanzania kwenda kuwekeza nchini Vietnam.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment