Utafiti
uliofanywa na Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na upimaji
wa virusi vya Ukimwi la MATUMAINI, unaonyesha kuwa kati ya wanawake kumi
wanaofanya biashara ya ngono wanaopima wanne kati yao wanakutwa na
virusi vya Ukimwi.
Mwenyekiti
wa Taasisi hiyo Bw. Onesmo Mwihava amesema wamekuwa wakifanya zoezi la
upimaji katika maeneo ya majumba ya starehe, baa na katika baadhi ya
madanguro yasiyo rasmi na kuwa licha ya kuwepo kwa jitihada za serikali
katika kutokomeza biashara ya ngono lakini wengi wa wanaojiuza wanakutwa
wameathirika ama kuwa na magonjwa ya zinaa.
Aidha,
Bw. Mwihava amesema kuwa watu wengi wamekuwa wakijihadhari na suala la
kupata mimba na kuacha kuchukua tahadhari kuwa katika kupata maambukizi
pamoja na magonjwa ya zinaa ambapo katika utafiti wao, kati ya watu kumi
waliojitokeza kupima kati yao sita huwa na magonjwa ya zinaa.
Ameongeza
kuwa mojawapo ya waathirika wakubwa wa ugonjwa wa ukimwi pamoja na
magonjwa ya zinaa ni vijana kutokana na kutochukua tahadhari kwa kufanya
ngono zembe na kuwa hali hiyo mara nyingi hutokana na kiwango cha fedha
alizotoa kwaajili ya huduma hiyo.
Mwihava
amezitaka taasisi na serikali kulivalia njuga suala la kutokomeza
biashara ya ngono pamoja na kutoa elimu kwa vijana na wanaojihusisha na
vitendo hivyo haswa baada ya kukamatwa kwakuwa kwa sasa wanawake hao
wengi wameanzisha mbinu mpya kwa kukaa katika baa na majumba ya starehe
na kutoka na wateja.
No comments:
Post a Comment