Sera ya Donald Trump ya kimataifa ni 'Marekani kwanza'.
Mgombea
urais kwa niaba ya chama cha Republican, Trump ambaye anaongoza hivi
sasa katika kinyang'anyiro hicho, amesema siasa zake za mambo ya nje,
zitaweka maslahi ya Marekani mbele.Katika mahojiano na gazeti la New York Times amesema nia yake sio kwamba anataka kuitenga Marekani ila anasema anapanga kusitisha kupunjwa kwa Marekani na washirika wake.
Amesema anataka Marekani iache kuendelea kununua mafuta yake kutoka Saudia hadi pale waSaudi watakapokubali kupeleka majeshi yao kupigana na wanamgambo wa IS.
Aidha Trump ameongeza kusema kuwa endapo ataibuka mshindi wa uchaguzi wa urais wa Marekani, atayaondoa majeshi ya Marekani kutoka Japan na Korea Kusini kama mataifa hayo hayatailipa zaidi Marekani kwa wanajeshi hao kuendelea weko nchini humo
No comments:
Post a Comment