Kutokana
na Tanzania kuwa na uchumi wa soko huria vijana wengi wameanza
kushiriki katika sekta isiyo rasmi hivyo kunawafanya kuchangia nusu ya
uchumi wa Taifa katika shughuli zao za kila siku.
Hayo
yamesemwa na mkurugenzi msaidizi wa Taasisi ya Soko la Ajira Ofisi ya
Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Ahmed Makbel wakati
akizungumza kuhusu mikakati mbalimbali na hatua zilizoanza kuchukuliwa
na serikali ili kuhakikisha inawainua vijana kiuchumi.
Makble
amezitaka taasisi zisizo za kiserikali kushirikiana na Serikali ili
waweze kutekeleza maagizo ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli na
kuhakikisha vijana wanafanya kazi zenye staha na kipato kizuri pamoja na
mazingira mazuri ya kazi.
Mkurugenzi
huyo amesema serikali imeanza kufanyia kazi baadhi ya mapendekezo ya
wadau wa maendeleo kuhusu kuwainua vijana kuanzia kwenye vipato vyao vya
kila siku sambamba na kuhakikisha fedha mbalimbali zinazotolewa na
serikali ziwafikie walengwa wa mifuko hiyo.
Makbel
ameongeza kuwa wahusika wakuu wa serikali kuanzia ngazi ya mtaa watoe
mazingira rafiki kwa vijana ili waone wao ni sehemu kubwa yakuchangia
pato la taifa na serikali kuu wameanza vikao vya pamoja ili waone
wanatekeleza vipi mipango ya kukuza uchumi wa vijana.
No comments:
Post a Comment