NEYMAR ATEMWA BRAZIL UNAMJUA MRITHI WAKE? - LEKULE

Breaking

27 Mar 2016

NEYMAR ATEMWA BRAZIL UNAMJUA MRITHI WAKE?

neymar-the-captain-brazil-1410970266783

neymar-the-captain-brazil-1410970266783 babu mkusa

Mshambuliaji  wa Barcelona na mlinzi wa PSG David Luiz wameachwa na timu yao ya taifa Brazil baada ya kusimamishwa kucheza mchezo wa  kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Paraguay hivyo kocha wa Brazil  Dunga amewaita wachezaji mbadala wa kuziba nafasi hizo mbili.

Kijana Gabriel Barbosa kutoka klabu ya Santos amechukua nafasi ya  nahodha wa Selecao Neymar katika kikosi kitakachokipiga na Paraguay.

Neymar alipata kadi ya njano ya tatu mfululizo kwenye michuano hiyo siku ya Ijumaa kwenye sare ya 2-2 dhidi ya Uruguay na atakosa mchezo wa pili wa Brazil dhidi ya Paraguay siku ya Jumanne

Gabriel ameichezea Brazil  chini ya miaka 17 , chini ya miaka 20 na chini ya miaka 23, kwasasa ana umri wa miaka 19 na  amekuwa akitazamwa na baadhi kama mrithi wa Neymar baada ya kuonesha mkubwa  ndani ya Santos.Gabriel-Barbosa-Almeida

Gabriel-Barbosa-AlmeidaNaye beki wa Corinthians ya huko Brazil Felipe pia amejumuishwa kwenye kikosi kitakachovaana na Paraguay kufuatia kusimamishwa kwa beki tegemeo David Luiz kwa kuwa na kadi sawa na Naymar.

No comments: