kiama kumfikia memphis depay mara ifikapo mwisho wa msimu kwa kutemwa na timu hiyo - LEKULE

Breaking

27 Mar 2016

kiama kumfikia memphis depay mara ifikapo mwisho wa msimu kwa kutemwa na timu hiyo


Winga wa Manchester United Memphis Depay ataondoka msimu huu hii imeripotiwa na ‘The sun’ kuwa winger huyo ameshindwa kufikia matakwa ya timu hiyo ya mji wa Manchester

Depay alitazamiwa kuwa ndiye mrithi wa Christiano Ronaldo kutokana na aina ya uchezaji wake alivyo kuwa PSV, alipewa jezi ya heshima ya timu hiyo namba 7 ambayo mastaa wote wa timu hiyo walivaa,Cantona,Beckham,Ronaldo na wengine wengi.

Depay amechemka kuonesha kiwango chake tangu afike klabuni hapo wakati mwingine anaweza kutoa pasi yenye kuigharimu timu yake kutokana kukaa na mpira muda mrefu kisha kuchukuliwa miguuni mwake.

Wengine wanao tazamiwa kuondoka msimu huu ni Marcos Roja ambae amecheza michezo 10 alie anza msimu huu,pamoja na Phil Jones ambae majeruhi yamemsonga.

Wakati hao wanaondoka kocha wa timu hiyo LOUIS Van Gal  nae ataona mlango wa kuondokea msimu ukiisha.

No comments: