Mambo matano ya kufahamu kuhusu Daraja la Kigamboni Dsm kabla ya kuanza kutumika siku 16 zijazo - LEKULE

Breaking

31 Mar 2016

Mambo matano ya kufahamu kuhusu Daraja la Kigamboni Dsm kabla ya kuanza kutumika siku 16 zijazo



Ujenzi wa daraja la Kigamboni ambalo linapita juu ya bahari ya hindi Dar es salaam kuwezesha wanaokwenda na kutoka Kigamboni kuvuka kwa urahisi bahari bila kutumia Pantoni, umekamilika kwa asilimia 90 na daraja litazinduliwa rasmi April 16 2016.
1. Kwenye eneo la daraja hili kuna kituo cha Polisi chenye mpaka mahabusu hivyo yeyote atakaezingua itakua rahisi kumshughulikia, pia kutakuwa na mizani ya kupimia magari mazito pamoja na ofisi ya kulitazama au kufatilia Daraja litakapoanza kutumika.
2.Watakaokuwa wanapita watakuwa wanalipia kuvuka kupitia daraja hilo ndio maana kuna ofisi au ‘vijiwe’ maalum ambavyo vitakua vinafanikisha process zote za kulipia.
3.Pamoja na kwamba bado daraja lenyewe halijaanza kutumika rasmi, Injinia anaesimamia ujenzi huo ameomba Watanzania kujali na kuthamini kila kilichopo kwenye daraja hilo na sio kuiba au kuharibu chochote, tayari mpaka sasa Camera nne za video za kurekodi mienendo na usalama wa daraja hilo zimeibiwa.
4.Ujenzi wa daraja hili ulianza February mwaka 2012 na walitarajia wangemaliza ujenzi January 31 2015 lakini ikashindikana sababu Wajenzi walipata changamoto katikati ya bahari, walichimba chini ya kitako cha bahari mita kama sitini na nne lakini walipofika kwenye mita 56 wakagundua kulikua na pango chini, wakaendelea kwenda chini mita 84.
5.Gharama za ujenzi kwa Mkandarasi ni shilingi za kitanzania BILIONI 214.6 ambazo kimkataba asilimia 25 zinalipwa kwa pesa za Kitanzania na asilimia 75 zinalipwa kwa dola za Kimarekani ambapo wakati wanafungua tenda Dola ya kimarekani ilikua shilingi 1590.

No comments: