Jumatatu ya March 28 timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ilikuwa inajiandaa kushuka dimbani kucheza mchezo wake wa nne wa kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika 2017 dhidi ya Chad, habari zilizotoka March 27 kutoka shirikisho la soka Afrika CAF ni kuwa Chad wamejitoa.
Baada ya Chad kujitoa kwa sababu za kutokuwa vizuri kiuchumi, CAF wamekumbushia sheria iliyowekwa January 15 2015, inaeleza kuwa kundi lolote litakalo salia na timu tatu, halitakuwa na best looser na badala yake kinara wa kundi ndio atakuwa anafuzu michuano hiyo pekee.
Kwa sheria za CAF michezo ya Chad inafutwa na msimamo wa Kundi G unabakia kuongozwa na Misri kwa point 4, Nigeria point 2 na Tanzania kubakia mkiani kwa kuwa na point moja, ikumbukwe kuwa Taifa Stars ilicheza na Chad March 23 N’Djamena na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
No comments:
Post a Comment