Mpira wa miguu ni mchezo wa aina yake na ndiyo mchezo pendwa kuliko yote
duniani. Baada ya mchezo wa kwa kawaida kuna matokeo ya aina tatu
kushinda, kufungwa na kutoka sare.
Watu wanatofautiana hisiakatika kupokea matokeo, tumekuwa tukishuhudia
hisia tofauti kutoka kwa mashabiki, wachezaji au makocha baada ya timu
zao kushinda au kupoteza michezo yao.
www.shaffihdauda.co.tz inakuletea top 10 ya matukio yaliyowafanya wachezaji wamwage machozi uwanjani.
10. Mario Balotelli– fainali ya Euro 2012
Mchezaji wa kimataifa wa Italia Mario Balotelli alilia kwenye mchezo wa
fainali za Euro mwaka 2012 baada ya timu yake kupoteza mchezo kwa bao
4-0 dhidi ya Hispania.
Alijikuta akiangua kilio pale aliposhuhudia nahodha wa Hispania Iker Casillas akinyanyua ndoo.
Jack Wilshere –Arsenal v Birmingham, fainali ya Carling Cup
Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere alijikuta akimwaga machozi pale Arsenal
iliporuhusu bao dakika ya 89 dhidi ya Birmingham City kwenye mchezo wa
fainali ya Carling Cup baada ya kutokea mkanganyiko kati ya Wojciech
Szczesny na Laurent Koscielny.
Goli hilo likazima kabisa ndoto za Arsenal kumaliza ukame wa aji kwenye kikosi chao.
Wachezaji pamoja na kocha wao walichanganyikiwa na kichapo hicho cha
dakika za lala salama. Ilikuwa ni miaka sita imepita tangu timu yao
ichukue kombe kwa mara ya mwisho na hiyo ilikuwa ngumu kukubali matokeo
hayo kwenye mchezo wa fainali.
8. Cristiano Ronaldo– fainali ya Euro 2004
Ni miaka 12 sasa tangu Cristiano Ronaldo aibuke kwenye kikosi cha timu
ya taifa ya Ureno. alikuwa na miaka 19 wakati Ugiriki wanaikandamiza
Ureno kwa bao 1-0 kwenye fainali ya michuano ya Euro iliyofanyika kwenye
ardhi ya kwao mwaka 2012. Baada ya filimbi ya mwisho, Ronaldo alikaa
chini na kuanza kumwaga machozi.
7. Ronaldinho–Atletico Mineiro
Ronaldinho alianza kulia baada ya kutupia kambani. Muda huohuo akapiga
magoti na kuanza kulia huku wachezaji wenzake wawakiwa wamemzunguka.
Lilikuwa ni tukuio la kushangaza, hasa kutoka kwa mchezaji maarufu wa aina yake ambaye hutabasamu muda wote akiwa uwanjani.
Kilio hicho kilitokana na majonzi aliyokuwa nayo Ronadinho kutokana na
kufiwa na baba yake wa kambo aliyefariki siku chache kabla ya mchezo
kutoka na shambulio la moyo (heart attack)
6. John Terry–Champions League nusu fainali
Baada ya kichapo cha bao 3-1 dhidi ya Atletico Madrid kwenye michuano ya
UEFA msimu wa 2013/24 hatua ya nusu fainali, nahodha wa Chelsea John
Terry alishindwa kuelewa ni kwa jinsi gani timu yake imetupwa nje ya
mashindano. Alishindwa kujizuia na kuanza kumwaga machozi.
5. Andrea Pirlo–Euro 2012 Final
Licha ya kuwa mchezaji aliyebarikiwa kiwango bora kwenye kikzazi chake
na kufanikiwa kutwaa karibu mataji yote muhimu, lakini kabati lake
halina taji la mataifa ya Ulaya (European Championships).
Mwaka 2012 alikaribia kutwaa kombe hilo na kuongeza la yale ya ligi ya Italia (Scudetto), Champions League na kombe la dunia.
Wakati wa michuano hiyo ambayo alitajwa kuwa man of the match kwenye
michezo mitatu huku timu yake ikifuzu hatua ya fainali lakini tukio
kubwa la kukumbukwa kwenye mashindano hayo ni ile penati aliyofunga
dhidi ya England katika changamoto za mikwaju ya penati.
Kwa bahati mbaya alishindwa kuisaidia timu yake ya taifa kutwaa taji
dhidi ya Hispania kwa kupoteza kwa bao 4-0 kwenye mchezo wa fainali.
Fundi huyo wa mpira alijikuta akifuta machozi kwa viganja vyake vya mikono licha ya kufanya mambo makubwa kwenye fainali hizo.
4. Luis Suarez–Liverpool v Crystal Palace, Premier League (2013/14)
Baada ya Crystal Place kupiga bao 3 ndani ya dakika 10 wakitoka nyuma
kwa bao 3-0 hadi sare ya magoli 3-3 dhidi ya Liverpool, nyota wa ‘Majooo
wa Jiji’ wakati huo Luis Suarez alijifunika uso kwa jezi yake huku
akilia.
Sare hiyo ilikuwa inafuta ndoto za Liverpool kushinda jombe la ligi ya
EPL kwa msimu huo. Msimu wa 2023-2014 ulikuwa ni msimu ambao Liverpool
walikaribia sana kushinda taji hilo kuliko wakati wowote.
“Ilikuwa inaumiza kukosa kombe la ligi. Huwezi kufungwa magoli matatu
ndani ya dakika 10. Sikuwahi kuduwazwa uwanjani kwa kiasi kile”, alisema
Suarez baada ya mchezo.
3.David Luiz – Brazil 2014, nusu fainali kombe la dunia
Akikongoza kikosi cha Brazil kama nahodha kwenye mchezo wa kombe la
dunia lakini alikiongoza kuyaaga mashindano hayo. Kukiongoza kikosi cha
Brazil ni ufahari lakini haikuwa hivyo kwa David Luis.
Mchezo ulimalizika huku Brazil ikibebeshwa zigo la magoli 7-1 na
Ujerumani na ikawa aibu kwake kuingoza nchi yake, alijikuta akibubujikwa
na machozi mbele ya mashabiki waliofurika uwanjani kuishangilia timu
yao wakiamini itafanya vizuri mbele ya wajerumani.
2. Iker Casillas– fainali ya Champions League 2014
Iker Casillas alishibwa kuzuia furaha yake wakati walipokaribia kuweka
rekodi ya kutwaa ubingwa wa Ulaya kwa mara ya 10 dhidi ya Atletico
Madrid kwenye mchezo wa fainali uliopigwa Lisbon.
Atletico waliibana Madrid na kujikuta ikishindwa kupata bao la
kusawazisha hadi dakika ya 92 baada ya Atletico kuwa mbele kwa bao 1-0.
Sergio Ramos aliisawazishia Madrid dakika ya 93 na kuufanya mchezo huo
kuongezewa dakika (extra time)
Mwisho wa siku Real Madrid ikashinda mchezo huo kwa bao 4-1 na kusherekea taji la 10 la Ulaya.
1.David Beckham – mechi yake yake ya mwisho PSG
Dakika ya 82 akiwa anafanyiwa mabadiliko kwenye mchezo wake wa mwisho
akiwa mchezaji wa Paris Saint Germain, David Beckham aliangua kilio
uwanjani.
Mashabiki 45,000 wakisimama kwa heshima kwa ajili ya nyota huyo wa
zamani wa timu ya taifa ya England, aliwakumbatia wachezaji wenzake
pamoja na wake wa timu pinzani kabla ya kutoka kumpisha Ezequiel
Lavezzi.
Baada ya mechi wachezaji wenzake walimchukua na kumrusha hewani kwa heshima.
No comments:
Post a Comment