● Aziagiza Halmashauri kushughulikia migogoro ya ardhi .
●
Azitaka kulisaidia Shirika la Nyumba ili lijenge nyumba za gharama
nafuu● Asema Halmashauri zinunue nyumba zinazojengwa na NHC kwa ajili ya
watumishi wao.
● Alipongeza NHC kwa kasi ya ujenzi wa nyumba bora katika Halmashauriza Miji na Wilaya.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline
Sylvester Lubala Mabula akisalimiana na Watumishi wa Hamashauri ya Mji
wa Buchosa alipowasili kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline
Sylvester Lubala Mabula akipewa maelezo na mtaalam wa mifumo ya uwekaji
kumbukumbu za umiliki wa ardhi alipotembelea idara ya ardhi Wilayani
Misungwi. Aliyoko katikati ni Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo Bw. Mshana.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline
Sylvester Lubala Mabula na Mbunge wa Chato Mhe.Dkt Medard Kalemani
wakikagua eneo la Kijiji cha Rusungwa lenye mgogoro mkubwa wa ardhi
unaofanya wananchi wa kijiji hicho kukosa ardhi ya kulima na uwekaji
huduma za jamii kama shule baada ya eneo la ekari 500 la kupewa
mwekezaji.
Meneja
wa NHC Mkoa wa Kagera Bw. Deogratius Batakanwa akimpewa maelekezo na
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline
Mabula ya kuhakikisha kuwa anatoa elimu ya kutosha itakayowezesha
wananchi, taasisi na Halmashauri ya Muleba kukamilisha ununuzi wa nyumba
zilizojengwa na NHC Wilayani Muleba.Naibu Waziri alitembelea nyumba
hizo na kulipongeza Shirika la Nyumba kwa ujenzi wa nyumba bora.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline
Sylvester Lubala Mabula akiwa katika picha ya pamoja na Madiwani wa
Halmashauri ya Muleba baada ya kuhutubia Baraza lao na kuliomba
liwezeshe ununuzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC
Wilayani humo. Pia aliagiza Baraza hilo kushiriki kikamilifu katika
kutatua migogoro mingi ya ardhi iliyoko katika Wilaya hiyo.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline
Sylvester Lubala Mabula akikagua nyumba zilizojengwa na NHC eneo la
Bombambili Mkoani Geita kwa ajili ya kuuza. Amewataka wananchi na
Halmashauri ya Mji wa Geita kununua nyumba hizo ili kuliwezesha Shirika
kuendelea kujenga nyumba katika Halmashauri zingine.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline
Sylvester Mabula akiwa na Mbunge wa Chato Mhe. Dkt Medard Kalemani
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini wakikagua nyumba za
gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Chato. Katika ziara hiyo
Naibu Waziri ameishauri Halmashauri ya Chato kununua nyumba hizo ili NHC
iongeze ujenzi wa nyumba zingine kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya
nyumba Wilayani humo.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline
Sylvester Lubala Mabula akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi za NHC
Mkoa wa Kagera alipotembelea na kusalimiana na wafanyakazi wa Shirika
hilo.
Meneja
wa NHC Mkoa wa Mwanza Injinia Benedict Kilimba akitoa maelezo ya mradi
wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Bombambili Geita, kwa
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline
Mabula alipotembelea mradi huo. Mhe. Naibu Waziri ameziagiza Halmashauri
nchini kusaidia uwekaji wa miundombinu kwenye maeneo ya ujenzi wa
nyumba hizo pamoja na kutoa ardhi bure kwa NHC ili nyumba zinazojengwa
ziwe na gharama nafuu kwa mnunuzi.
Mkuu
wa Wilaya ya Misungwi Bibi Mwajuma Nyiruka akitoa taarifa ya sekta ya
ardhi ya Wilaya yake kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula alipoitembelea
Halmashauri ya Misungwi kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi.
Baraza
la Madiwani Muleba wakimsikilza Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula (hayuko pichani)
alipohutubia Baraza hilo.
No comments:
Post a Comment