Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Ramadhan Mwinyi akifungua rasmi Mkutano wa JPC kati ya Tanzania na Zambia. |
Sehemu ya maofisa wa Serikali ya Zambia wakifuatilia Mkutano. |
Sehemu ya maofisa wa Serikali ya Tanzania wakifuatilia Mkutano.
Serikali
za Tanzania na Zambia zinakutana katika kikao cha siku mbili kujadili
na kukubaliana maeneo ya ushirikiano ambayo watayasimamia kwa
pamoja kwa lengo la kuongeza kasi ya maendeleo ya nchi hizo mbili.
Kikao hicho kinachojulikana kama Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano
kati ya Tanzania na Zambia (JPC) kinafanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano
wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuanzia leo.
Katika
hotuba yake ya ufunguzi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje,
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Ramadhan
Muombwa Mwinyi alieleza kuwa uhusiano wa Tanzania na Zambia ni mzuri na
kufanyika kwa kikao hicho ni uthibitisho dhahiri.
Aidha, Balozi Mwinyi alieleza kuwa kufanyika kwa kikao hicho kunatoa fursa kwa wajumbe kuchambua kwa pamoja hatua zilizofikiwa na changamoto zilizojitokeza
katika utekelezaji wa maeneo yaliyoafikiwa wakati wa kikao cha 8 cha
JPC kilichofanyika Lusaka Juni 2006. Maeneo hayo ni pamoja na biashara,
viwanda, mawasiliano, uchukuzi, nishati, uhamiaji, kilimo, elimu,
michezo, madini, utalii, maliasili na utamaduni.
“Haya
ni baadhi ya maeneo ambayo nchi zote mbili zinayapa umuhimu mkubwa ili
kuharakisha maendeleo ya pande zote mbili Katika majadiliano yetu
tutalenga zaidi maeneo haya ili tubuni utaratibu mzuri wa kushirikiana
katika utekelezaji kwa lengo la kuleta tija kwa nchi na wananchi wake”.
Balozi Mwinyi alifafanua.
Kwa
upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimaendeleo na
Mashirika ya Kimataifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Zambia, Bw,
Sylevester Mundanda alieleza kuwa Tanzania na Zambia zimejaliwa kuwa na
maliasili lukuki kama vile ardhi, madini, maji na wanyama pori, hivyo,
endapo kama zitatumiwa vizuri zinaweza kubadilisha uchumi wa nchi hizo
kwa ajili ya kuwaletea maisha bora wananchi wake.
Alisisitiza
umuhimu wa kukubaliana maeneo machache ya kipaumbele na kuyawekea
mikakati ya utekelezaji na ubunifu bila kusahau kujiwekea utaratibu wa
kupima ufanisi kila baada ya muda.
Bw,
Mundanda alihitimisha kwa kusema kuwa vikao vya JPC ni fursa nzuri
kujadili changamoto za kiuchumi na kubuni mikakati ya pamoja kukabiliana
nazo ili uchumi uweze kukua kwa faida ya wananchi wa pande zote.
|
No comments:
Post a Comment