Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (watatu kulia) akiwa na
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR)
nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole (wapili kushoto), Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia), Naibu
Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya
Wakimbizi, Harrison Mseke (wapili kulia) wakielekea katika hafla fupi
iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa ajili ya kumuaga Mwakilishi wa UNHCR
nchini, iliyofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam
leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza katika hafla ya
kumuaga Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi
(UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole (watatu kulia).
Katika hotuba yake fupi, Waziri Kitwanga alimshukuru Mwakilishi huyo
kwa ushirikiano wake mzuri kati ya Wizara na UNHCR, pia alimtakia safari
njema na mafanikio mema arudipo nyumbani kwake. Joyce anatarajia
kustaafu rasmi katika nafasi hiyo mwezi ujao. Wanne kulia ni Naibu
Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni, kushoto aliyekaa ni Katibu
Mkuu, Meja Jenerali Projest Rwegasira, na Naibu Katibu Mkuu, Balozi
Simba Yahya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimkabidhi zawadi
ya picha Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi
(UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole, kwa ajili ya
kumbukumbu yake kutokana na ushirikiano mzuri kati ya Shirika lake la
UNHCR na Wizara. Hafla hiyo fupi ya kumuaga iliyoandaliwa na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi ilifanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es
Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini,
anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole akimshukuru Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wapili kushoto) pamoja na viongozi
wengine wa Wizara hiyo, kwa ushirikiano mkubwa waliompa wakati
anaiongoza UNHCR. Pia katika hotuba yake, Joyce alimpongeza Rais John
Magufuli kwa uongozi wake mzuri pamoja na ushirikiano mkubwa wanaoupata
kutoka katika Serikali yake. Wakwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Watatu kushoto ni Katibu Mkuu wa
Ofisi ya Makamu wa Rais, Mbarak Abdulwakil ambaye aliwahi kuwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Wapili kulia ni Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, na Wanne
kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrsion Mseke. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkurugenzi
wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrsion Mseke
akizungumza katika hafla ya kumuaga Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake,
Joyce Mends-Cole (watatu kulia). Katika hotuba yake, Mseke alimshukuru
Joyce kwa ushirikiano wake mkubwa aliouonyesha wakati wa uongozi wake.
Wapili kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga
ambaye aliiongoza hafla fupi iliyofanyika katika Hoteli ya Serena,
jijini Dar es Salaam. Wanne kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo,
Injinia Hamad Masauni. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja
Jenerali Projest Rwegasira. Watatu kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya
Makamu wa Rais, Mbarak Abdulwakil ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu,
Balozi Simba Yahya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kushoto)
akimuaga Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi
(UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole mara baada ya
kumaliza sherehe fupi iliyoandaliwa na Wizara ya kumuaga kiongozi huyo
wa UNHCR. Hafla hiyo fupi ilifanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar
es Salaam leo na kuhudhuriwa na Viongozi Wakuu wa Wizara akiwemo Waziri
wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wanane kushoto), Naibu Waziri
wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni (watano kulia), Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wasaba kushoto), Katibu
Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mbarak Abdulwakil ambaye aliwahi kuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (wanne kulia), Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya
(wanne kushoto), Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia
Wakimbizi (UNHCR) nchini, anayemaliza muda wake, Joyce Mends-Cole
(wasita kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Wizara pamoja
wa UNHCR mara baada ya hafla fupi ya kumuaga Joyce, iliyofanyika katika
Hoteli ya Serena, Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment