Na RFI
Rais wa
Misri Abdel Fattah al-Sisi amekubali kwa mara ya kwanza Jumatano hii
kwamba ndege ya watalii ya Urusi ambayo iliangushwa Oktoba 31 katika
eneo la Sinai na kuua watu wote 224 waliokuemo, kilikua kitendo cha
shambulio, kama ilivyoelezwa mapema na Urusi.
Tawi la
kundi la Islamic State nchini (IS) lilikiri kuhusika na shambulio hiyo
siku hiyo hiyo, na kuthibitisha baadaye kwamba ilikuabomu dogo
lililowekwa ndani ya ndege hiyo, lakini mpaka wakati sasa Cairo ilikua
ikisema na kurejelea kwamba sababu za ajali hazijulikani.
"Yeyote
yule alieidungua ndege hiyo, alikua anatafuta nini? Kuwashambulia tu
watalii (nchini Msri)? Hapana, kuweka hatarini uhusiano wetu na Urusi,"
Rais Sissi amesema mbele ya umati wa viongozi wa serikali na biashara
wakati wa mkutano kuhusu maendeleo ya Misri, mkutano ambao umerushwa
hewani kwenye runinga mbalimba nchini Misri.
Siku kumi
baada ya ajali, Moscow, kupitia sauti ya Rais Vladimir Putin mwenyewe,
alitangaza kuwa wapelelezi wake kwenye eneo la tukio walibaini kwamba
ndege hiyo iliangushwa kwa shambulio, na kupiga marufuku ndege zote za
Urusi kusafiri kwenda Misri hadi itakapotangazwa tena. Uingereza ilipiga
marufuku ndege zake zote kusafiri kwenda kituo cha mapumziko cha Sharm
el-Sheikh, ambapo ndege ya Urusi iliruka ikipaa hewani. Wakati huo huo
Uingereza kama Urusi, iliwarejesha nyumbani raia wake wote waliokuwepo
katika mji huo wa mapumziko.
Sekta ya
Utalii, ambayo tayari imekabiliwa na wimbi la mashambulizi nchini Misri
iko hatarini. London, mpaka sasa haijaruhusu ndege zake kusafiri kwenda
katika mji wa Sharm el-Sheikh, wala Moscow kuruhusu ndege zake kusafiri
kwenda nchini Misri.
No comments:
Post a Comment