Waziri wa
Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
(kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Ufundi, Aksante wakati akimwelezea
juhudi zinazoendela za kukarabati jengo la watoto ambalo lipo Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya Rais John Pombe Magufuli
alivyoagiza. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla akimsikiliza mkururugenzi
huyo. Leo Waziri Mwalimu na naibu waziri wa wizara hiyo, Dk Kigwangalla
wametembelea Jengo la Watoto na Jengo namba mbili la wazazi kukagua
utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli ambaye ametaka jengo la
watoto linalovuja likarabatiwe haraka.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Professa
Lawrence Mseru akifafanua jambo mbele ya Waziri Mwalimu na Naibu Waziri
wa wizara hiyo Dk Kigwangalla kuhusu utekelezaji wa agizo la Rais
Magufuli alilolitoa hivi karibuni.
Waziri wa
Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
(katikati), Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk Hamisi Kigwangalla
wakitazama jengo (pichani halipo) ambalo limeaanza kukarabariwa baada ya
agizo la rais.
Waziri
Ummy Mwalimu na naibu waziri wake, Dk Kigwangalla wakimsikiliza Naibu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali (MNH), Professa Museru katika wodi ya
wagonjwa wa figo waliolazwa katika jengo la watoto ambalo limeanza
kukarabatiwa.
Waziri Ummy Mwalimu akimsikiliza mmoja wa wagonjwa wa figo waliolazwa katika jengo la watoto.
Waziri wa
Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akizungumza na mmoja wa watoto wanaougua ugonjwa wa saratani waliolazwa
katika jengo la watoto lililopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
(MNH). Picha zote na John Stephen-Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
Na Neema Mwangomo-PRO- MNH
Waziri wa
Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo
ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- kwa lengo la kukagua jengo
la watoto pamoja na jengo la wazazi namba mbili ( Maternity Block Two)
ili kuona utendaji kazi na utekelezaji wa maagizo ya Rais John
Magufuli .
Mwishoni
mwa wiki iliyopita, Rais Magufuli aliagiza watumishi wa Wizara ya Afya
, Maendeleo ya Jamii , Jinsia , wazee na Watoto kitengo cha afya ya
mama na mtoto kuhama katika jengo hilo ili kupisha Hospitali ya Taifa
Muhimbili kulitumia kama wodi ya wazazi .
Waziri
Ummy ambaye ameambatana na Naibu Waziri Dokta Hamis Kigwangala
ameelezea kuridhishwa na ukarabati unaoendelea katika majengo hayo .
“Jengo la
watoto tatizo kubwa lilikuwa ni miundombinu ya maji lakini naona
ukarabati unaendelea vizuri na nina imani kuwa ukarabati utakamilika kwa
wakati” amesema Waziri .
Akizungumzia
kuhusu jengo la wazazi namba mbili , Waziri huyo wa afya amesema kuwepo
kwa jengo hilo ni faraja kwa kina mama na kusisitiza kwamba hakuna
mama mjamzito atakayelala chini .
Mpaka sasa kina mama 53 tayari wamehamia katika jengo hilo na wanapatiwa huduma zote.
No comments:
Post a Comment