Wahamiaji
wakipanga foleni kwa kusubiri wapewe chakula, katika mji wa Gevgelija
kwenye mpaka kati ya Makedonia na Ugiriki Februari 24, 2016.
Na RFI
Mvutano
mkubwa kati ya Ugiriki na Austria umeleta athari Alhamisi hii katika
mkutano wa nchi za Umoja wa Ulaya mjini Brussels. Mkutano ambao unalenga
kukomesha hali inayojitokeza dhidi ya ongezeko la wahamiaji. Hali hii
inaweza kuzua mgogoro mkubwa wa kibinadamu.
Umoja wa
Ulaya unaonyooshewa kidole na nchi kadhaa zikiongozwa na Austria
umelaumiwa kwa kutolinda vya kutoosha mpaka wa nje wa Umoja huo ambapo
wakimbizi wengi wamekua wakipitia kwa kuingia katika ardhi yake, Ugiriki
imejibu kwa hasira wakati wa mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Ndani
kutoka nchi 28 wanachama wa Umoja wa Ulaya.
"Austria
inatuchukulia kama maadui," Waziri wa mambo ya Ndani wa Ugiriki Yannis
Mouzalas ameshangaa mbele ya wenzake, kwa mujibu wa chanzo cha
kidiplomasia, na wakati huo huo, Athens imemuitisha balozi wake mjini
Vienna kwa "mashauriano."
"Ugiriki
haitokubali kuwa Lebanon ya Ulaya," Bw Mouzalas ameonya, huku akieleza
kwamba wakimbizi wa Syria sasa wanawakilisha robo ya wakazi wa hiyo.
Ugiriki
inahisi kweli kwamba inaendelea kujiangamiza yenyewe. Tangu mapema mwezi
Januari, zaidi ya wahamiaji 102,000 waliingia nchini humo wakipitia
katika bahari ya Mediterranean, kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la
Wahamiaji (IOM).
Ugiriki
imezidiwa kuzidiwa ikilinganishwa na mpango wa kugawanya wahamiaji
wanaoomba hifadhi waliowasili katika nchi hiyo wakitokea nchi ingine za
ulaya. Wakimbizi wasiopungua 600 "wameonekana" nchini Italia na Ugiriki
katika miezi ya hivi karibuni kwa jumla ya 160,000 ambao wanapaswa
kuwepo katika nchi hizi katika kipindi cha miaka miwili.
Na uamuzi
wa Makedonia kukataa kuwapa njia raia Afghanistan kwenye mpaka wake na
Ugiriki, na kuamuru raia wa Syria na Iraq kuonyesha vitambulisho vya
uraia, imeiongezea Ugiriki kazi kubwa na hivo kutumbukia katika hali ya
sintofahamu ya wakimbizi.
No comments:
Post a Comment