Shambulio la risasi laua kadhaa Marekani - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Friday, 26 February 2016

Shambulio la risasi laua kadhaa Marekani


Shambulio latokea Hesston

Watu kadhaa wameuawa na wengine thelathini kujeruhiwa katika kwa risasi magharibi mwa jimbo la Kansas nchini Marekani.
Maafisa wa polisi wamesema mwanaume aliyepiga risasi hizo ameuwawa baada ya shambulio lililotokea katika mji wa Hesston.
Mkuu wa polisi wa kituo cha eneo hilo T.Walton amesema polisi wanafuatilia uhalifu uliotokea na kuna uwezekana kuwa na majeruhi zaidi.
"hili ni tukio la kutisha na baya lililowahi kutokea katika mji wa wilaya Harvey na Hesston Newton.Limesambaa nje na tafadhali mtuvumilie wakati tunaendelea kulitatua tatizo hilo.Mnapaswa kuwa makini,tunaenda kujaribu kupata taarifa zote kwa hali na mali,kuna wengi ambao watakutana na majonzi kabla ya haya yote kuisha" alisema mkuu huyo wa Polisi
shuhuda mmoja ameeleza alichokiona na kukisikia..

''yote ambayo ninayajua ni kwamba niliona watu wakikimbia na nikadhani walikuwa wanakimbia moto,hivyo nikasogea hatua chache na kusikia milio ya risasi na watu zaidi wakikimbia na milio hiyo ilizidi na mimi pia nikaanza kukimbia'
Post a Comment