Katibu mkuu wav Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon baada ya mazungumzo yake pamoja na rais Pierre Nkurunziza
Viongozi 5
wa Afrika wameanza ziara ya siku mbili mjini Bujumbura Burundi kujaribu
kuwatanabahisha rais Pierre Nkurunziza na upande wa upinzani waanzishe
majadiliano ili kuupatia ufumbuzi mzozo uliopo.
Rais
Jacob Zuma wa Afrika Kusini ameshawasili katika mji mkuu wa Burundi
Bujumbura,akiongoza ujumbe wa Umoja wa Afrika ulioamuliwa kuundwa
viongozi wa Umoja huo walipokutana mwishoni mwa mwezi wa january
uliopita mjini Addis Abeba. Mbali na rais Zuma,ujumbe huo wa Umoja wa
Afrika unawaleta pamoja marais wa Mauritania Mohammed Ould Abdel
Aziz,Macky Sall wa Senegal,Ali Bongo Ondimba wa Gabon na waziri mkuu wa
Ethiopia Haile Mariam Dessalegn.
Mara
baada ya kuwasili viongozim hao wa nchi tano za Umoja wa Afrika
wamekwenda kuweka mashada ya mauwa kwenye makaburi ya wahanga wa
demokrasia,ikiwa ni pamoja na lile la rais wa kwanza kuchaguliwa kwa
njia za kidemkorasia nchini humo Melchior Ndadaye.
Kuwasili
ujumbe huo wa viongozi wa mataifa ya Afrika mjini Bujumbura ni sehemu ya
juhudi jumla za kidiplomasia za kujaribu kusaka ufumbuzi wa amani kwa
mzozo wa Burundi.(P.T)
Thibitisho la serikali kwa Ban Ki-Moon
Katibu
mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban-Ki-Moon,ambae binafsi alikuwa zirani mjini
Bujumbura jumatatu na jumanne wiki hii,alihakikisha kwamba amepatiwa
thibitisho na rais Pierre Nkurunziza kwamba mjadala utakaozihusisha
pande zote utaanzishwa nchini humo.
Juhudi za
awali za majadiliano zilishindwa kwasababu serikali ya Burundi haikuwa
ikitaka kuzungumza na baadhi ya vyama vya upinzani.
"Viongozi
wa mataifa ya Afrika wanakuja kujadiliana na serikali pamoja na
wahusika wengine kuhusu namna ya kuanzisha mdahalo wa pande zote,"
amesema mwanadiplomasia mmoja wa kiafrika aliyeko mjini Bujumbura na
ambae hakutaka jina lake lijulikane.
Suala la wanajeshi wa Afrika halizungumziwi
"Mada ya kutumwa kikosi cha nchi za Afrika haimo katika ajenda ya mazungumzo" ameongeza kusema mwanadiplomasia huyo.
Umoja wa
Afrika uliamua mwezi decemba mwaka jana kutuma kikosi cha wanajeshi 5000
nchini Burundi ili kuzuwia wimbi la matumizi ya nguvu. Lakini uamuzi
huo ulikabiliwa na upinzani mkubwa wa rais Pierre Nkurunziza pamoja pia
na viongozi kadhaa wa Afrika katika mkutano wao wa kilele mwezi Januari.
Burundi
imetumbukia katika mzozo wa kisiasa na kugubikwa na matumizi ya nguvu
tangu rais Pierre Nkurunziza alipotangaza kugombea mhula wa tatu mwezi
wa aprili mwaka 2015.
Matumizi
ya nguvu yaliyofuatia yameangamiza maisha ya zaidi ya watu 400 na zaidi
ya 240.000 kuihama nchi hiyo. Mashirika yanayopigania haki za binaadamu
yanazungumzia kuhusu kuwepo makaburi ya jumla,visa kadhaa vya watu
kuuliwa kiholela,mauwaji yaliyolengwa na kudai ufanyike uchunguzi wa
kimataifa kuhusu madai hayo.
No comments:
Post a Comment