Hello

Welcome lekule blog

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation.
together in the world. #lekule86
Join us on

Wabunge Wa CCM Waungana Na Upinzani Kuibana Serikali Kuhusu Ujenzi Wa Reli, Kuhamiashia Hela BoT Na Shirika la Ndege ATCLBila kujali itikadi za vyama vyao, wabunge wameukosoa mwongozo wa kuandaa mpango wa Bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha wa 2016/17, wakihoji suala la ujenzi wa reli ya kati kwa viwango vya kimataifa pamoja na mambo mbalimbali.

Pia, wamepinga mpango wa Serikali wa kutaka mapato yote ya halmashauri, taasisi na mashirika ya umma kuwekwa kwenye mfuko mkuu wa Serikali na kuitaka itafute vyanzo vipya vya mapato.

Katika kuonyesha msimamo wa pamoja, wabunge wote wanaotokea mikoa ambayo Reli ya Kati inapita wameunda umoja kuhakikisha Serikali katika mpango wake wa bajeti ya 2016/17, inakuja na mwelekeo wa ujenzi wa reli ili nchi ipate maendeleo ya kweli, si ya kwenye makabrasha.

Umoja huo uko chini ya uenyekiti wa Ezekiel Maige, mbunge wa Msalala (CCM), wakati Zitto Kabwe, ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo), anakuwa katibu wa wabunge hao walio katika mikoa inayoanzia Dar es Salaam kupitia Tabora hadi Mwanza na kutokea Tabora hadi Kigoma.

Mikoa mingine inayounganishwa na reli hiyo kongwe ni Shinyanga, Morogoro na Dodoma.

Akichangia mjadala kuhusu mwongozo huo, Zitto alitahadharisha dhidi ya siasa za kikanda.

“Tunapaswa kuwa makini sana kwenye siasa za kikanda. Tusikubali maslahi ya nchi nyingine yafunike maslahi ya nchi yetu. Ni lazima tuhakikishe mtandao wa reli ambao utaisaidia nchi yetu,” alisema kiongozi huyo wa chama cha ACT-Wazalendo.

“Juzi nilisikia kwamba tuna tatizo la fedha. Mwaka jana Bunge lilipitisha sheria ya Kodi ya Maendeleo ya Reli ambayo inataka kila mzigo unaoingia nchini, utozwe asilimia 1.5 kwa ajili ya reli. Tunacho chanzo cha uhakika cha fedha na tunachopaswa kufanya ni kuhakikisha kwamba chanzo hiki kinatumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa.

“Tupewe tafsiri ya Reli ya Kati. Kwetu sisi Reli ya Kati ni ile inayotoka Dar es Salaam, Tabora, Uvinza (kwenda msongati Burundi). Kutoka Kaliua kwenda Mpanda mpaka Kalema kwa ajili ya ujenzi wa Bandari ya Kalema. Kutoka Isaka kwenda Keza Ngara kwa ajili ya madini ya Nikel yaliyogundulika huko ili kusafirishwa kwenda Dar es Salaam.”

Mvutano kuhusu reli ulianza tangu wiki iliyopita katika mjadala wa hotuba ya Rais John Magufuli wakati mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe aliposema atawashawishi wenzake kuigomea bajeti ya 2016/17, iwapo Serikali haitatoa mwelekeo wa ujenzi wa reli hiyo ya kati.

Kuhusu Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Zitto alisema badala ya Serikali kukimbilia kununua ndege mbili, inapaswa kulifanyia shirika hilo marekebisho kwa kuzifanya taasisi za utalii kuwa na hisa ATCL.

“Kutokana na wingi wa watalii wanaoingia nchini, Tanapa na Ngorongoro wanapata mapato. Turuhusu wawe na hisa ATCL ili shirika hili lijiendeshe kibiashara,” alisema Zitto.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba aliungana na Zitto kumtaka Waziri wa Fedha, Dk Philip Mpango aeleze Reli ya Kati itajengwa kuanzia wapi kwenda wapi wakati atakapokuwa akiwasilisha mpango huo.

Alisema bila kuwa na reli ya uhakika ni ndoto nchi kupata maendeleo inayoyatarajia.

Serukamba alisema kuna taasisi zilizoanzishwa kwa sheria hivyo kuzitaka zianze kupeleka fedha katika mfuko mkuu wa Serikali, italazimika sheria kubadilishwa.

Mbunge huyo alihusisha suala hilo na uvivu wa watendaji wa hazina kutopenda kufikiria vyanzo vipya vya mapato. 

“Mtazifanya halmashauri zishindwe kujiendesha jamani mbona hamfikirii suala hili. Waziri hii kitu si sawa kabisa iondoeni,” alisema.

“Viwango vya kodi mnavyoviweka ni vikubwa sana. Hivi (Mamlaka ya Mapato) TRA haijifunzi kwa nchi kama Mauritius ambayo viwango vyake vya kodi ni vidogo lakini inakusanya fedha nyingi?” alihoji.

Naye mbunge wa Kigamboni (CCM), Dk Faustine Ndugulile alisisitiza umuhimu wa kuwa na reli.

“Tukitaka kupaisha uchumi, lazima tuwe na Reli ya Kati ya kiwango cha kisasa. Ni lazima serikali mje na mpango wa kueleweka,” alisema akizungumzia reli hiyo ambayo ujenzi wake ulianza mwaka 1905 wakati nchi ikiwa chini ya wakoloni wa Kijerumani.

Mbunge wa viti maalum (CCM), Mwanne Nchemba alisema suala la reli ya kati si la mzaha kwa maelezo kuwa wapigakura wengi wanaitegemea reli hiyo, pia ni njia nzuri ya kusafirisha mizigo, hivyo lazima Serikali ihakikishe inaijenga kwa kiwango cha kisasa.

Kwa upande wake mbunge wa Kasulu Mjini (CCM), Daniel Nsanzugwako alisema sera ya uchumi wa viwanda ya Serikali ya Awamu ya Tano haiwezi kufanikiwa vyema bila nchi kuwa na reli ya uhakika.

“Mizigo lazima ipite katika reli ili kuokoa barabara zetu. Msipokuja na mkakati hatutawaelewa katika bunge hili. Haiwezekani miaka 20 sasa tunazungumzie reli tu,” alisema huku akisisitiza kuwa uwepo wa reli utaongeza kasi ya mapato bandarini.

Mbunge wa Babati Mjini (Chadema), Pauline Gekul naye aliungana na Serukamba kuhoji uamuzi huo wa Serikali kuweka fedha zote za mapato kwenye mfuko wa Serikali, akisema utaua halmashauri.

“Tukumbuke historia ya ugatuaji wa madaraka, kumbukeni jinsi Mwalimu (Julius)Nyerere alivyourudisha baada ya kuona faida zake. Serikali za mitaa zina mamlaka ya kukusanya mapato na kutumia, sasa hayo mamlaka mnayaondoa mnategemea nini,” alisema.

“Mkipitisha suala hili, haya mapato hayatakusanywa ipasavyo na pia mtatengeneza mianya mingine ya ajabu ajabu.Tumekuwa tukiona jinsi ambavyo Serikali inashindwa kutoa fedha za maendeleo, sasa mnapotaka fedha zote zipelekwe katika mfuko mkuu wa Serikali, je zitatoka zote wakati zitakapohitajika?” alihoji.

Gekul alisema kama tatizo ni sheria za halmashauri na taasisi, ni vyema zinakabadilishwa ila si kuziondolea mapato.

Mbunge wa Nsimbo (CCM), Richard Mbogo alizungumzia Shirika la Ndege (ATCL) akitaka lipunguze wafanyakazi wake ili kuweza kujiendesha kibiashara.

Alisema kwa sasa shirika hilo linasuasua kutokana na kutokuwa na mapato ya kutosha.

Share this:

ABOUTME

Hi all. This is deepak from Bthemez. We're providing content for Bold site and we’ve been in internet, social media and affiliate for too long time and its my profession. We are web designer & developer living India! What can I say, we are the best..

Post a Comment
My photo

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
My goal with BLOG is to help you learn Electrical.

Labels

LEKULE TV EDITORIALS ARTICLES DC ROBOTICS DIGITAL SEMICONDUCTORS GENERATOR AC EXPERIMENTS MANUFACTURING-ENGINEERING REFERENCE FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY ELECTRONICS ELECTRICAL ENGINEER MEASUREMENT TRANSDUCER & SENSOR VIDEO ARDUINO RENEWABLE ENERGY AUTOMOBILE TEARDOWN SYNCHRONOUS GENERATOR DIGITAL ELECTRONICS ELECTRICAL DISTRIBUTION CABLES AUTOMOTIVE MICROCONTROLLER SOLAR PROTECTION DIODE AND CIRCUITS BASIC ELECTRICAL ELECTRONICS MOTOR SWITCHES CIRCUIT BREAKERS CIRCUITS THEORY PANEL BUILDING ELECTRONICS DEVICES MIRACLES SWITCHGEAR ANALOG MOBILE DEVICES WEARABLES CAMERA TECHNOLOGY COMMUNICATION GENERATION BATTERIES FREE CIRCUITS INDUSTRIAL AUTOMATION SPECIAL MACHINES ELECTRICAL SAFETY ENERGY EFFIDIENCY-BUILDING DRONE CONTROL SYSTEM NUCLEAR ENERGY SMATRPHONE FILTER`S POWER BIOGAS BELT CONVEYOR MATERIAL HANDLING RELAY ELECTRICAL INSTRUMENTS ENERGY SOURCE PLC`S TRANSFORMER AC CIRCUITS CIRCUIT SCHEMATIC SYMBOLS DDISCRETE SEMICONDUCTOR CIRCUITS WIND POWER C.B DEVICES DC CIRCUITS DIODES AND RECTIFIERS FUSE SPECIAL TRANSFORMER THERMAL POWER PLANT CELL CHEMISTRY EARTHING SYSTEM ELECTRIC LAMP FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 2 BIPOLAR JUNCTION TRANSISTOR 555 TIMER CIRCUITS AUTOCAD BLUETOOTH C PROGRAMMING HOME AUTOMATION HYDRO POWER LOGIC GATES OPERATIONAL AMPLIFIER`S SOLID-STATE DEVICE THEORRY COMPUTER DEFECE & MILITARY FLUORESCENT LAMP INDUSTRIAL ROBOTICS ANDROID ELECTRICAL DRIVES GROUNDING SYSTEM CALCULUS REFERENCE DC METERING CIRCUITS DC NETWORK ANALYSIS ELECTRICAL SAFETY TIPS ELECTRICIAN SCHOOL ELECTRON TUBES FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 1 INDUCTION MACHINES INSULATIONS USB ALGEBRA REFERENCE HMI[Human Interface Machines] INDUCTION MOTOR KARNAUGH MAPPING USEUL EQUIATIONS AND CONVERSION FACTOR ANALOG INTEGRATED CIRCUITS BASIC CONCEPTS AND TEST EQUIPMENTS DIGITAL COMMUNICATION DIGITAL-ANALOG CONVERSION ELECTRICAL SOFTWARE GAS TURBINE ILLUMINATION OHM`S LAW POWER ELECTRONICS THYRISTOR BOOLEAN ALGEBRA DIGITAL INTEGRATED CIRCUITS FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 3 PHYSICS OF CONDUCTORS AND INSULATORS SPECIAL MOTOR STEAM POWER PLANTS TESTING TRANSMISION LINE C-BISCUIT CAPACITORS COMBINATION LOGIC FUNCTION COMPLEX NUMBERS CONTROL MOTION ELECTRICAL LAWS INVERTER LADDER DIAGRAM MULTIVIBRATORS RC AND L/R TIME CONSTANTS SCADA SERIES AND PARALLEL CIRCUITS USING THE SPICE CIRCUIT SIMULATION PROGRAM AMPLIFIERS AND ACTIVE DEVICES APPS & SOFTWARE BASIC CONCEPTS OF ELECTRICITY CONDUCTOR AND INSULATORS TABLES CONDUITS FITTING AND SUPPORTS ELECTRICAL INSTRUMENTATION SIGNALS ELECTRICAL TOOLS INDUCTORS LiDAR MAGNETISM AND ELECTROMAGNETISM PLYPHASE AC CIRCUITS RECLOSER SAFE LIVING WITH GAS AND LPG SAFETY CLOTHING STEPPER MOTOR SYNCHRONOUS MOTOR AC METRING CIRCUITS BECOME AN ELECTRICIAN BINARY ARITHMETIC BUSHING DIGITAL STORAGE MEMROY ELECTRICIAN JOBS HEAT ENGINES HOME THEATER INPECTIONS LIGHT SABER MOSFET NUMERATION SYSTEM POWER FACTORS REACTANCE AND IMPEDANCE INDUCTIVE RECTIFIER AND CONVERTERS RESONANCE SCIENTIFIC NOTATION AND METRIC PREFIXES SULFURIC ACID TROUBLESHOOTING TROUBLESHOOTING-THEORY & PRACTICE 12C BUS APPLE BATTERIES AND POWER SYSTEMS DC MOTOR DRIVES ELECTROMECHANICAL RELAYS ENERGY EFFICIENCY-LIGHT INDUSTRIAL SAFETY EQUIPMENTS MEGGER MXED-FREQUENCY AC SIGNALS PRINCIPLE OF DIGITAL COMPUTING QUESTIONS REACTANCE AND IMPEDANCE-CAPATIVE SEQUENTIAL CIRCUITS SERRIES-PARALLEL COMBINATION CIRCUITS SHIFT REGISTERS WIRELESS BUILDING SERVICES COMPRESSOR CRANES DIVIDER CIRCUIT AND KIRCHHOFF`S LAW ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS 1 ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS B ELECTRICAL TOOL KIT ELECTRICIAN JOB DESCRIPTION INDUSTRIAL DRIVES LAPTOP SCIENCE THERMOCOUPLE TRIGONOMENTRY REFERENCE UART oscilloscope BIOMASS CONTACTOR ELECTRIC ILLUMINATION ELECTRICAL SAFETY TRAINING ELECTROMECHANICAL FEATURED FILTER DESIGN HARDWARE JUNCTION FIELD-EFFECT TRANSISTORS NASA NUCLEAR POWER VALVE COLOR CODES ELECTRIC TRACTION FLEXIBLE ELECTRONICS FLUKE GEARMOTORS INTRODUCTION LASSER PID PUMP SEAL ELECTRICIAN CAREER ELECTRICITY SUPPLY AND DISTRIBUTION MUSIC NEUTRAL PERIODIC TABLES OF THE ELEMENTS POLYPHASE AC CIRCUITS PROJECTS REATORS SATELLITE STAR DELTA VIBRATION WATERPROOF