Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na Balozi wa Uingereza hapa nchini Bi. Dianna Melrose Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiagana na Balozi wa Uingereza hapa nchini Bi. Dianna Melrose Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na Balozi Mteule wa Namibia hapa nchini Bi Theresia Samaria
mara baada ya kupokea Hati ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana Balozi Mteule wa Namibia hapa nchini Bi Theresia Samaria
mara baada ya kupokea Hati ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na Balozi wa Misri hapa nchini Mohamed Yasser El Shawaf
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiagana na Balozi wa Misri hapa nchini Mohamed Yasser El Shawaf Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule kutoka Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC) Jean Pierre Mutamba Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini Thamsanqa Mseleku
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU
Uingereza
Imempongeza Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli Kwa Jitihada Zinazofanywa Na Serikali Yake Katika Ukusanyaji Wa
Mapato Na Kukabiliana Na Vitendo Vya Rushwa.
Akizungumza
Baada Ya Kukutana Na Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar Es Salaam
Leo,Balozi Huyo Mh Dianna Melrose Amesema Juhudi Za Mapambano Dhidi Ya
Ufisadi Pamoja Na Kubana Matumizi Na Ubadhirifu Wa Mali Za Umma
Kunakotekelezwa Kwa Vitendo Na Serikali Ya Awamu Ya Tano Ni Mfano Wa
Kuigwa.
Balozi
Melrose Amesema Waziri Mkuu Wa Nchi Ya Uingereza Bw. David Cmeroon
Amevutiwa Na Utendaji Kazi Wa Rais Magufuli Na Kusisitiza Kwamba Nchi
Hiyo Itaendeleza Ushirikiano Wa Karibu Uliopo Kati Ya Uingereza Na
Tanzania Katika Nyanja Mbalimbali Za Maendeleo………………….Mh Dianna Melrose
Balozi Wa Uingereza Hapa Nchini
Kabla Ya
Kukutana Na Balozi Wa Uingereza Hapa Nchini Rais Magufuli Amekutana Na
Kufanya Mazungumzo Na Balozi Wa Afrika Ya Kusini Hapa Nchini Mh
Thamsanqa Mseleku,Na Balozi Wa Misri Hapa Nchini Mh Mohamed Yasser El
Shawaf Ambao Amewahakikishia Kuwa Serikali Yake Ya Awamu Ya Tano
Itaendeleza Ushirikiano Mzuri Uliopo Kati Yake Na Nchi Hizo Hususani
Katika Kukuza Biashara Na Kuwanufaisha Wananchi Wa Pande Zote.
Katika Hatua Nyingine Rais Magufuli Amepokea Hati Za Utambulisho Kutoka Kwa Mabalozi Wawili.
Mabalozi
Waliokabidhi Hati Zao Za Utambulisho Ikulu Jijini Dar Es Salaam Ni Mh
Jean Pierre Mutamba Tshampanga Wa Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo Na Mh
Theresia Samaria Wa Namibia.
Rais
Magufuli Amewaeleza Mabalozi Hao Kuwa Tanzania Itaendelea kushirikiana
Na Nchi Hizo Katika Nyanja Mbalimbali Hususani Katika Uchumi.
Wakati
Huo Huo Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
Amekutana Na Kufanya Mazungumzo Na Rais Mstaafu Wa Awamu Ya Nne Dkt
Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu Jijini Dar Es Salaam.
No comments:
Post a Comment