Mwenyekiti
wa Bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) Prof
Moses Warioba(wa kwanza kushoto) akitoa tamko la kumsimamisha kazi
Mhariri mtendaji wa kampuni ya magazeti ya serikali Bw.Gabriel Nderumaki
(hayupo pichani) kutokana na utendaji usiorizisha.Wengine pichani ni
wajumbe wa Bodi hiyo Dkt Evelyn Richard na Bw.Alfred Nchimbi(Picha na
Daudi Manongi)
Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo mhe Nape Nnauye akiongea na vyombo
vya Habari kuhusu maagizo aliyoyatoa kwa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni
ya magazeti ya serikali TSN ikiwemo sababu za wafanyakazi wengi kuacha
kazi katika shirika hilo.
Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akitembezwa
kuonyeswa mazingira ya kampuni ya magazeti ya serikali(TSN) jana jijini
Dar es Salaam.Kulia ni mhariri mtendaji wa kampuni hiyo ya magazeti ya
serikali Bw.Gabriel Nderumaki ambaye amesimamishwa kazi kutokana na
utendaji usiorizisha na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya
wakurugenzi ya kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) Prof Moses Warioba.
Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipata maelezo
jinsi gazeti linavyotengenezwa kutoka kwa mchapaji msaidizi wa magazeti
ya serikali (TSN) Bw.Paul Kasele alipofanya ziara katika shirika hilo
jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisaini kitabu cha
wageni wakati alipotembelea kampuni ya magazeti ya serikali TSN jana
jijini Dar es Salaam.
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Bodi ya
wakurugenzi wa magazeti ya Serikali,(TSN) imemsimashisha kazi Mhariri
Mtendaji wa magazeti hayo Bw Gabrieli Nderumaki kupisha uchunguzi
kutokana na utendaji usioridhisha ndani ya kampuni hiyo.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw Prof Moses Warioba
amesema hatua za kumsimamisha kazi Mhariri Mtendaji huyo umetokana na
kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo
ambapo nafasi yake itachukuliwa na Naibu Mhariri Bi Tumma Abdalah.
“Kumekuwa
na mambo mengi yanayofanyika bila kufuata utaratibu ndani ya kampuni
hii ikiwemo wafanyakazi kutoelewana na menejimenti katika kulipwa
stahili zao, pamoja na wafanyakazi kupewa majukumu ambayo hawana uwezo
wa kuyatekeleza”.Alisema Prof Warioba.
Aidha
Prof Warioba ametengua uteuzi wa Bw Felix Mushi aliyekuwa Meneja mauzo
na masoko katika kiwanda cha uzalishaji kwa kukosa sifa na utendaji
mbovu uliopelekea kampuni kushuka katika uzalishaji.
Hatua
hiyo ya kuwawajibisha watendaji hao imetokana na Ziara ya Mhe. Nape
Nnauye Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika Kampuni hiyo
ambapo pia hakuridhiswa na utendaji mbovu uliopelekea wafanyakazi
21 kuacha kazi.
“Nataka
Bodi itafakari juu ya malalamiko yaliopo kwa wafanyakazi na wachukue
hatua kabla mimi sijakutana na wafanyakazi hao wiki ijayo ili kujua
mapungufu yako wapi.”Alisema Mhe Nape.
Hata
hivyo Bodi hiyo ya wakurugenzi inaendelea kutafuta namna ya kuboresha
utendaji ndani ya kampuni ili iendane na kasi iliyopo katika
uzalisahaji wa magazeti kwa kiwango kikubwa
No comments:
Post a Comment