Marekani na Urusi zimetangaza kusimamisha vita nchini Syria kuanzia usiku wa Ijumaa.
Makubaliano hayo yametangazwa baada ya mawasiliano kwa njia ya siku kati ya Rais Barack Obama na mwenzake Vladimir Putin.
Mjumbe
maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria, Staffa de Mistura amesema
changamoto kubwa ni kuhakikisha makubalino ya kuacha vita yanatekelezwa
katika uwanja wa vita.
Makundi mawili ya wapiganaji wenye itikadi kali ya kiislamu Islamic State na Al- Nusra Front hayapo kwenye makubaliano hayo.
Muungano
wa upinzani nchini Syria umesema kujihusisha kwao kutategemea jinsi gani
serikali ya Syria na washirika wake watakavyoacha kuuzingira,
kuwafungulia wafungwa na kuacha kupiga mabomu.
Mwandishi
wa BBC wa masuala ya kidiplomasia anasema ukurasa huu mpya kutaipa
ugumu Urusi kuwapiga mabomu wapinzani ambao sio waislamu wanaungwa mkono
na mataifa ya Magharibi na baadhi ya nchi maarufu za Kiarabu.BBC
No comments:
Post a Comment