Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua baadhi ya nyumba za dharura wanazoishi
wananchi wa katika kijiji cha Kasanga baada ya maeneo yao kukumbwa na
mafuriko kwenye tarafa za Pawaga na Idodi, Iringa Februari 22, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mkuu Kassim Majaliwa akikagua eneo yalipojengwa makazi ya dharura
katika kijiji cha Kasanga ili kuwahifadhi wananchi walioathirika kwa
mafuriko katika tarafa za Pawaga na Idodi Iringa Februari 22, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akiwapa pole wanawake na watoto wakati
alipotembelea makazi ya dharura waliyojengewa na serikali katika kijiji
cha Kasanga wanapohifadhiwa waathirika wa mafuriko yaliyozikumba
tarafa za Pawaga na Idodi , Iringa Februari 22, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akiwapa pole wanawake na watoto wakati
alipotembelea makazi ya dharura waliyojengewa na serikali katika kijiji
cha Kasanga wanapohifadhiwa waathirika wa mafuriko yaliyozikumba
tarafa za Pawaga na Idodi , Iringa Februari 22, 2016.Kushoto ni Mbunge
wa Ismani na Wairi w Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William
Lukuvi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akiwapa pole wanawake na watoto wakati
alipotembelea makazi ya dharura waliyojengewa na serikali katika kijiji
cha Kasanga wanapohifadhiwa waathirika wa mafuriko yaliyozikumba tarafa
za Pawaga na Idodi , Iringa Februari 22, 2016. (Picha na Ofisi ya

Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea taarifa ya msaada kutoka kwa meneja
uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mangele katika mkutano wa
kuwapa pole wananchi wa tarafa za Pawaga na Idodi uliohutubiwa na Waziri
Mkuu katika Kijiji cha Kasanga, Iringa Februari 22, 2016. Mfuko huo
umetoa mabati 200 na saruji mifuko 200 vyote vikiwa na thamani ya sh.
6,600,000/=.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi
ya watoto wanaoishi katika makazi ya dharura kwenye kijiji cha Kasanga
wanapohifadhiwa waathirika wa mafuriko yaliyozikumba tarafa za Idodi na
Pawaga, Iringa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati
alipotembelea kijiji hicho kuwapa pole wananchi Februari 22, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amepokea misaada mbalimbali yenye thamani ya sh.
milioni 85.88/- kwa ajili ya wananchi walioathirika na mafuriko kwenye
vijiji vya kata ya Mlenge, tarafa ya Pawaga, wilaya ya Iringa vijijini
mkoa wa Iringa.
Misaada
hiyo imetolewa na wadau mbalimbali kutokana na mafuriko ambayo
yalibomoa nyumba 82 katika kitongoji cha Kilala, kijiji cha Kisanga na
kuwaacha wananchi wake bila makazi.
Akizungumza
na wananchi wa kijiji cha Kasanga ambako alikwenda kukagua athari za
mafuriko na kuwapa pole wananchi hao leo mchana (Jumatatu, Februari 22,
2016), Waziri Mkuu aliwashukuru wadau wote waliojitolea kuwachangia
watu waliopata maafa kutokana na mafuriko hayo.
Wadau waliotoa misaada hiyo ni Benki ya NMB mabati 500, mifuko ya saruji 500, kilo 820 za maharage, kilo 750 za unga wa mahindi na lita 250 za mafuta ya kupikia vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 20/-. Wengine ni Mfuko wa Pensheni wa PPF uliotoa mabati 200 na mifuko ya saruji 200 vyenye thamani ya sh. milioni 6.6/-.
Wengine ni Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) waliotoa mabati 200 na mifuko ya saruji 160 vyenye thamani ya sh. milioni 4.5/-; Kiwanda cha kusindika nyanya cha RedGold kimetoa mifuko ya saruji 100 na mabati 50 vyenye thamani ya sh. Milioni 3/-; mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya CHADEMA, Bi. Susan Chogisasa na wenzake wametoa mabati 150, mifuko 23 ya saruji, kilo 100 za maharage, kilo 50 za chumvi na nguo mbalimbali vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 1.3/-.
Madiwani wa Iringa Vijijini walitoa sh. 380,000/-, Wabunge wa Viti Maalum kupitia CCM walitoa vifaa vya sh. Milioni 1.7/-; ofisi ya CCM Mkoa wametoa vifaa vya sh. milioni 6.1/-, Kamanda wa UVCCM Mkoa wa Iringa, Bw. Salim Abri aliipatia Halmashauri ya Wilaya ya Iringa sh. milioni 5/- ili wanunue vyakula vya waliopatwa na maafa.
Naye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni mbunge wa Isimani, Bw. William Lukuvi alitoa fedha taslim sh. milioni 20/- kati ya hizo sh. milioni 15 zikiwa ni zake na milioni 5/- ni za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Bw. George Simbachawene. Pia alikabidhi seti 251 za mashuka zenye thamani ya sh. milioni 4/- zikiwa ni mchango kutoka Benki ya CRDB.
Waziri Lukuvi ambaye alishatoa mabati 250, aliahidi kuongeza mabati mengine 250 (yote yana thamani ya sh. milioni 8), pia alikabidhi sh. milioni 1.5/- kwa diwani wa Mlenge ili ziwasaidie kukodi gari la kukarabati barabara yao ambayo imeharibika sana kutokana na mafuriko hayo.

Mapema,
akitoa taarifa ya maafa kwa Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bi.
Amina Masenza alisema jumla ya kaya 82 zilikosa makazi kutokana na mvua
zilizonyesha Februari 12 na kusababisha mafuriko. Kabla ya hapo, kaya
nyingine 75 zenye wakazi 377ziliathirika kutokana na mvua zilizoanza
Februari 3, mwaka huu.
Alisema
miundombinu ya barabara na ya maji safi iliharibiwa vibaya na
kusababisha hasara ya zaidi ya sh, milioni 250/-. Pia wakazi hao
walikubwa na uginjwa wa kipindupindu kutokana na mto Mapogoro kufurika
na kusomba baadhi ya vyoo vya wakazi hao.
“Tangu
Februari mosi, wamekwishapokea wagonjwa wa kipindupinda 351 lakini
walioko wodini hivi sasa ni wagonjwa 25 tu,“ alisema Mkuu huyo wa mkoa.
No comments:
Post a Comment