Polisi auwa na majambazi TangaAskari wa jeshi la polisi Koplo George Braiton aliyepigwa risasi na majambazi wakati akikabiliana nao katika tukio la ujambazi lililotokea barabara ya sita na saba jijini Tanga amefariki dunia.

Koplo Braiton amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Tanga,Bombo, akiwa na watu wengine wawili waliopigwa risasi katika tukio hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga ACP.Mihayo Msikhela amesema kuwa bastola ilitumika kupoteza uhai wa Koplo George Braiton wa kituo cha polisi Chumbageni na kujeruhi raia wengine wawili ambao bado wanaendelea na matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga.

Polisi wamesema walifanikiwa kuwakamata majambazi hao wakiwa na bastola waliyoitumia kwenye tukio hilo pamoja na visu wanavyovitumia kwenye matukio ya kihalifu.

Majirani waliokuwa wakiishi na Koplo Braitoni wamesema tukio hilo limewagusa,lakini wakaiomba jamii kuwafichua wahalifu kwa lengo la kukabiliana na vitendo hivyo.

Kolpo Braitoni anatarajiwa kusafirishwa kupelekwa mkoani Mara Februari 16 kwa ajili ya mazishi.
Post a Comment
My photo

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
My goal with BLOG is to help you learn Electrical.
Powered by Blogger.