Katika
mkesha wa mkutano wa kimataifa hapo kesho Alhamisi jijini Munich kuhusu
kuzindia mchakato wa amani nchini Syria, Uturuki imeendelea kufungia
mpaka wake ma mia ya wakimbizi wanaokimbia mapingano ya majeshi ya
serikali na waasi katika mji wa Aleppo.
Mji wa
munichi nchini ujerumani unawapokea kesho wajumbe wa kimataifa
wanaojumuika katika nchi 17 na mashirika ya kimataifa waliokubaliana
mwezi Novemba mwaka 1015 jijini Vienna kuhusu dira ya kidiplomasia
kuhusiana na mzozo wa Syria.
Mpango
huo ulianzishwa kupitia azimio la baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
la Desemba 18, linaloomba pia uwepo wa mazingira ya mashirika ya misaada
kufika katika maeneo ya miji iliozingirwa, pamoja na usitishwaji
mapigano.
Kufuatia
mkutano huo, serikali ya Washington imeiomba kwa mara nyingine tena
Urusi inayosaidia kijeshi mashambulizi ya Utawala wa rais Assad
kusitisha mara mara moja hususan katika jimbo la Aleppo.
Waziri wa
mambo ya nje wa Marekani John Kerry ambae serikali yake inajitahidi
kuwa karibu na serikali ya Moscou kwa ajili ya kupatikana kwa suluhu ya
mgogoro wa Syria amesema wanaelekea Munich wakiwa na matumaini makubwa.
Mzozo wa
Syria uliodumu sasa ni zaidi ya miaka 5, uliogharimu maisha ya watu
takriban laki mbili na elfu sitini na kuwafanya wengine zaidi ya milioni
moja kutoroka makwao.(VICTOR)
Kabla ya
uzinduzi wa mkutano huo mratibu wa muungano wa upinzani nchini Syria
Riyad Hijab atakutana jumatano hii jijini London na waziri wa mambo ya
nje wa Uingereza Philip Hammond.
Wakati
huo huo jijini Moscou itazinduliwa ofisi ya wawakilishi ya wakurdi wa
Syria wanaoomba kuwakilishwa katika mazungumzo, jambo ambalo
linatupiliwa mbali na serikali ya Ankara.
Na huko
Hegue nchini Uholanzi waziri mkuu wa Uholanzi Mark Rutte atampokea
waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu na kuzungumzia kuhusu suluhu ya
mgogoro wa wakimbizi.
Swala
hili litajadiliwa pia katika mkutano wa mawaziri wa nchi za kujihami wa
nchi za magharibi Nato jijini brussels hii leo. Wajumbe katika mkutano
huo watajadili pia kuhusu ombi la Ujerumani na Uturuki kuitaka Nato
kuingilia kati mgogoro huo.
Waziri wa
ulinzi wa Marekani Ashton Carter atajaribu kukazia muungano wa majeshi
kuhusu kupambana na kundi linalojiita Islamic State linalotumia fursa ya
mapigano kati ya serikali na waasi kukalia maeneo makubwa ya Syria.
No comments:
Post a Comment