Waziri wa
mambo ya nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo ameliambia baraza la Seneti
hapo jana kwamba, Rwanda haiwezi kuwafukuza wakimbizi wa Burundi kwa
muda wote hali ya wasiwasi itaendelea kuripotiwa nchini humo.
Mushikiwabo amesema waliokimbilia nchini Rwanda kutoka Burundi, inamaana
kuwa wanamatatizo na serikali ya Burundi, hivyo kuwafukuza nchini
Rwanda mbali na kuwa ni kinyume na mila na tamaduni za Rwanda lakini pia
ni kinyume na sheria za Kimataifa.
Akizungumza
hapo jana Louise Mushikiwabo amesema tangu Rwanda ilipoanza kuwapokea
wakimbizi kutoka nchini Burundi, kumekuwa na maswala chungu nzima ambayo
yamekuwa yakiibuka, na hata ripoti nyingi zimekuwa zikitolewa, hilo ni
jambo la kawaida.
Mushikiwabo
amesema kinachosikitisha ni kuona badala ya kuutafutia suluhu mzozo wa
Burundi, hali imekuwa ikiendelea kuwa mbaya huku ripoti zikiendelea
kutolewa bila kujali madhila yanayo wakumba wananchi.
Mushikiwabo,
ameendelea kukanusha madai kwamba imekuwa ikiwasaidia wapinzani wa rais
Nkurunziza kwa kuwapa mafunzo ya kijeshi vijana wanaokabiliana
kuipindua serikali iliopo sasa nchini Burundi.
Hivi
karibuni ripoti iliovuja ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa ilieleza kuwa
serikali ya Rwanda inawapa mafunzo vijana waliokimbilia nchini Rwanda na
ambao wanajiandaa kuishambulia serikali ya rais Nkurunziza.
Mushikiwabo
amesema tatizo kubwa lililopo ni kuendelea kupuuzia mzozo, vinginevyo
kuna uwezekano wa kuupatishia suluhu mzozo uliopo ili kuepukana na
lawama za kila wakati.CHANZO:RFI
No comments:
Post a Comment