Waziri wa
mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius amejiuzulu wadhifa huo . Bwana
Fabius ambae pia aliwahi kuwa Waziri Mkuu ameteuliwa kuwa Rais wa Baraza
la Katiba la Ufaransa.
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius
Maafisa
wa serikali nchini Ufaransa wamethibitisha leo kwamba Waziri Fabius
amejiuzulu wadhifa wake na kwa maana hiyo ameamua kujiondoa kwenye siasa
za mstari wa mbele baada ya kuwamo katika medani hiyo kwa miaka zaidi
ya 30.
Bwana
Fabius alionekana akiwapungia watu wakati alipokuwa anatoka kuhuduhuruia
kikao chake cha mwisho cha baraza la mawaziri leo asubuhi. Mwenyewe
amethibitisha kwamba amejiuzulu wadhifa wake, hatua itakayosababisha
kufanyika mabadiliko ya baraza la mawaziri baadae mnamo wiki hii.
Muda
mfupi tu baada ya kujiuzulu ,Rais Francois Hollande alimteua kuwa Rais
wa Baraza la Katiba, chombo kikuu cha mamlaka ya katiba nchini Ufaransa.
Hata hivo msemaji wa serikali ameeleza kwamba bwana Fabius ataendelea
kuwamo katika serikali, madhali bado hajapitia kwenye tume za
kumthibitisha kuwa rais wa baraza hilo.
Baraza la mawaziri kubadilishwa
Waziri Fabius kwenye mkutano juu ya tabia nchi
Kujiuzulu
kwa bwana Fabius kutafuatiwa na mabadiliko ya baraza la mawaziri
yatakayompa Rais Francois Hollande fursa ya kuijenga upya timu
atakayoingia nayo katika uchaguzi wa rais utakaofanyika mwaka ujao
nchini Ufaransa.
Bwana
Fabius mwenye umri wa miaka 69 alikuwa Waziri Mkuu kijana kuliko wengine
wote katika historia ya Ufaransa. Aliushika wadhifa huo wakati akiwa na
umri wa miaka 37 mnamo mwaka wa 1984.
Katika
wadhifa wa waziri wa mambo ya nje bwana Fabius alishiriki katika
mazungumzo yaliyoleta makubaliano baina ya Iran na mataifa sita makubwa
juu ya mpango wa nyuklia wa nchi hiyo. Miongoni mwa mafanikio yake pia
ni kufikiwa mkataba wa kimataifa juu ya tabia nchi .
Bwana
Fabius alikuwa mwenyekiti wa mazungumzo ya wiki mbili yaliyofanyika
mjini Paris yaliyowezesha kufikiwa kwa mkataba huo. Licha ya kuitwa
msoshalisti wa mvinyo, mara nyingine, Fabius ameweza kuthibitisha
umahiri katika siasa za kimataifa.
Lakini
siyo bila ya kuandamwa na kashfa. Baada ya majasusi wa Ufaransa
kubainika, baada ya meli ya walinzi wa mazingira ,Rainbow Worrior
kuzamishwa nchini New Zealand Fabius alikiri baadae kwamba meli hiyo
ilizamishwa kwa kupigwa bomu na majasusi wa Ufaransa. Hapo awali
serikali ya Ufaransa ilikanusha kuhusika na tukio hilo.
Meli hiyo ilikuwa njiani kuwapeleka wanaharakati waliokuwa wanakwenda kupinga kufanyika majaribio ya nyuklia.CHANZO:DW
No comments:
Post a Comment