Mbunge wa
Mafinga Vijijini, Cosato Chumi (Mwenye diary mkononi) akipata maelekezo
katika kiwanda cha kiwanda cha Sao Hill katika ziara ya kutembelea
Taasisi Binafsi na za Umma.
Mbunge wa Mafinga Vijijini, Cosato Chumi (wa pili kutoka kushoto)akionyeshwa shughuli zinazofanywa katika kiwanda cha Sao Hill.
Wengine ni Denis kutemile anayefuatia na Hezron Vuhahula ambaye ni katibu wa mbunge.
Baadhi ya wafanyakazi wa sao hill wakiwa kazini.
Sehemu ya nguzo zinazozalishwa na kiwanda cha Sao Hill.
MBUNGE
wa Mafinga Vijijini, Cosato Chumi amefanya ziara kutembelea Taasisi za
Umma na Binafsi kwa kutembelea Sao Hill Industries, Sao Hill Forest,
Kiwanda cha Pareto na kampuni ya simu ya TTCL.
Katika
ziara hiyo mbunge ametembelea Vituo vya Polisi, Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (PCCB), NSSF , Bank za Mucoba, NMB na CEDB,Magereza
,pamoja na Taasisi za Elimu.
Amesema kufanya ziara ni kujitambulisha, kufahamiana na kufahamu changamoto wanazokabiliana nazo.
Chumi
amesema nguzo za umeme, kutoka Afrika Kusini sio sahihi wakati
zinaweza kupatikana na uwezo wa kuzalisha nguzo 90000 kwa mwaka.
Amesema
kutokana na maelezo ya kiwanda hicho na wamesema ikiwa watapata nafasi
ya kuongezewa uwezo wa kuvuna kutoka Shamba la Taifa la Msitu wa Sao
Hill, wanaweza kusambaza nguzo zaidi.
Mgao
wa kuvuna wa cubic 120,000 Changamoto ni kuwa wakipewa kitalu lakini
ndani ya kitalu sio kila mti unafaa kwa nguzo kwa hiyo ombi lao, wapewe
kwa mfumo wa kwamba wavune kile ambacho kinafaa kwa nguzo harafu miti
inayofaa labda kwa karatasi ibaki kwa ajili ya Kiwanda cha mgololo.
wakati huohuo wawekezaji Mafinga waiomba Tanesco kuwafungia laini madhubuti ya Umeme katika kiwanda cha Pareto ambacho kiko chini ya Kampuni ya Pyrethrum Company of Tanzania (PCT).
No comments:
Post a Comment