Mkurugenzi
Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga(katikati) akizungumzia mbele ya
waandish wa habari (hawapo pichani) ni kwa jinsi gani wamepata
malalamiko kutoka kwa familia zinazofanyiwa unyanyasaji wa kijinsia hasa
ubakaji na ulawiti katika ngazi za mahakama, polisi na baadhi ya
hospitali hapa nchini.
Mratibu
wa Kituo cha usuluishi cha TAMWA, Bi. Gladness Hemedi Munuo akizungumza
mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati walipokuwa
wakilaani vikali ucheleweshwaji na upotoshaji wa kesi za vitendo vya
ukatili.
Mtoto akitoa ushaidi ni kwa jinsi gani alivyofanyiwa kitendo cha ukatili wa kijinsia.
Mwanasheria
wa TAWLA, Mary Richard (wa kwanza kulia) akizungumza ni kwa jinsi gani
wanavyowasaidia wanawake wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia
leo katika mkutano na waandishi wa habari leo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini.
CHAMA
cha Wanahabari wanawake nchini Tanzania(TAMWA) kimelaani vikali
ucheleweshwaji na upotoshwaji ushahidi wa kesi za vitendo vya ukatili wa
kijinsia hasa ubakaji na ulawiti katika ngazi ya mahakama, polisi na
baadhi ya madaktari hospitalini. Hali hiyo imekuja baada ya TAMWA
kubaini kesi sitini na mbili (62) za ubakaji zimeshindwa kutolewa hukumu
au uamuzi na mahakama mbalimbali jijini Dar es Salaam katika kipindi
cha mwaka 2014 hadi 2015.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Edda Sanga
amesema kati ya kesi 63 za ubakaji, ni kesi moja tu mtuhumiwa
amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, kesi arobaini na tatu (43) bado
ziko mahakamani, kesi kumi na saba (17) zimeshindwa kufika mahakamani
ambapo kesi mbili zimefutwa kwa kukosa ushahidi.
Pia
aliongezea kwa kusema kuwa uongozi wa TAMWA umesikitishwa kuona kesi
hizo zikicheleweshwa na vyombo mbalimbali vya serikali ikiwemo jeshi la
polisi na mahakama. Na kuna baadhi ya viongozi wanapokea rushwa ili
kuzima kesi za watoto wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia, pia baadhi ya
polisi wamekuwa wakishindwa kutoa ushirikiano kwa mlalamikaji ambapo
wanatoa maneno ya vitisho na kupelekea mlalamikaji kukosa ujasiri wa
kuhifadhi na kutetea kesi yake na wakati mwingine mama mzazi anaandikwa
kama mlalamikaji badala ya mtoto mwenyewe aliyefanyiwa ukatili huo.
Pia
wameunga mkono tamko la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliposema wakati wa siku ya sheria
duniani kuwa "Kila Hakimu wa Mahakama anapaswa kuhukumu kesi si chini ya
260 kwa kila mwaka na kwa haki", Hivyo basi wao kama TAMWA wanaamini
ndani ya mwaka huu Mahakama hapa nchini zitafanya kazi yao kiweledi ili
kuweza kupunguza ukatili wanaofanyiwa watoto wa kike.
No comments:
Post a Comment