Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kimemtaka Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Jecha Salum Jecha ajiuzulu wadhifa huo kutokana na hatua aliyochukuwa ya kufuta uchaguzi na kutangaza tarehe ya kurudiwa bila kufuata sheria hivyo kumemuondolea sifa ya kusimamia na kuongoza tume hiyo.
Tamko hilo limetolewa jijini Dar es Salaam na Kaimu MkurugenziMtendaji wa LHRC Bi Imelda Urrio ambapo amesema ukosefu wa taarifa sahihi na rasimi za michakato ya maridhiano toka kufutwa kwa uchaguzi kunaondoa imani ya wananchi juu ya viongozi wao, tume na mchakato mzima wa chaguzi za kidemokrasia Zanzibar.
Amesema kuwa kufutwa na kutangazwa upya kwa uchaguzi wa Zanzibar kunakiuka katiba,sheria,na kanuni za uchaguzi na pia misingi ya demokrasia ya utawala wa sheria nchini.
Amesema kuwa katiba ya Zanzibar na sheria za uchaguzi hazijampa mamlaka mwenyekiti na hata tume yote kufuta uchaguzi na hivyo kilichotokea Zanzibar kimeaacha watanzania wakiwa hawaelewi ni sheria na katiba ipi imetumika kufuta uchaguzi huo.
Bi Imelda ameongeza kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 123 cha sheria ya uchaguzi Zanzibar mtu akishachaguliwa uchaguzi wake hautohojiwa isipokuwa kwa kupeleka shauri mahakamani,hivyo kwa msingi huo LHRC wanaona kwamba hakuna kifungu chochote cha sheria kinachoipa tume ya uchaguzi au mwenyekiti wake mamlaka ya kufuta uchaguzi na kuamuru marudio isipokuwa kwa amri ya mahakama.
Wakati huohuo chama cha kijamii CCK kimemsimamisha kazi na uanachama naibu katibu mkuu wake wa Zanzibar Ali Khatib Aliambaye pia alikuwa mgombea urais wa Zanzibar kwenye uchaguzi uliotangazwa kufutwa na ZEC Oktoba 2015.
Mwenyekiti wa CCK Costantine Achitanda amesema chama kimefikia maamuzi hayo ili kupisha uchunguzi dhidi yake kufuatia uamuzi wake binafsi wa kutangazia umma kuwa CCK itashiriki uchaguzi wa marudio huko Zanzibar kinyume na taratibu za chama.
Mwenyekiti wa CCK Costantine Achitanda amesema chama kimefikia maamuzi hayo ili kupisha uchunguzi dhidi yake kufuatia uamuzi wake binafsi wa kutangazia umma kuwa CCK itashiriki uchaguzi wa marudio huko Zanzibar kinyume na taratibu za chama.
Wakili Hamis Mkindi kutoka LHRC akiongea.Kushoto ni kaimu mkutugenzi wa kituo cha sheria na Haki za binadamu Bi Imelda Lulu Urrio
Waandishi wa habari wakifuatilia habari hiyo.
No comments:
Post a Comment