Viongozi wa Dini Wazidi Kutofautiana Kuhusu Sakata La Zanzibar.......Sheikh Ponda Issa Ponda Apinga Uchaguzi Kurudiwa ZanzibarMgogoro kuhusu kurudiwa kwa uchaguzi viswani Zanzibar unazidi kupasua nchi, sasa viongozi wa Dini ya Kiislam wametofautiana.

Ikiwa ni siku moja baada ya Alhad Mussa Salum ambaye ni Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam kuunga mkono Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar (ZEC) kutangaza tarehe ya uchaguzi visiwani humo, Jumuiya ya Taasisi za Kiislam Tanzania imepinga.

Sheikh Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu nchini katika mkutano wake na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam amesema, kuruhusu kurudiwa kwa uchaguzi visiwani humo ni kupandikiza mbegu za chuki kwa wananchi.

Sheikh Ponda amesema kuwa uchaguzi uliofanyika Oktoba mwaka jana haukuwa na mashaka kwa kuwa, waangalizi wa nje pia walithibitisha hilo.

“Ripoti za waangalizi wa ndani na nje zilithibitisha kuwa uchaguzi haukuwa na dosari. Kuna sababu gani ya kurudia uchaguzi,” amehoji Sheikh Ponda.

Wakati Sheikh Ponda akihoji sababu za ZEC kutaka kurudiwa kwa uchaguzi huo, Sheikh Alhad aliipongeza tume hiyo na kuongeza“tunaiomba ZEC kusimamia kazi hii kwa haki, uadilifu na umakini mkubwa…”

Sheikh Alhad jana alisema kuwa Baraza la Waislam Tanzania (BAKWATA) linaunga mkono uamuzi wa ZEC kurudia uamuzi huku akikitaka Chama cha Wananchi (CUF) ambacho kimesusia uchaguzi huo, kushiriki.

CUF kwenye mkutano wake wa Baraza Kuu uliofanyika tarehe 27 na 28 Januari mwaka huu kilieleza kususia uchaguzi huo uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi mwaka huu na kudai kuwa, hakuna sababu yoyote kwa chama hicho kushiriki. ZEC ilifuta uchaguzi huo tarehe 28 Oktoba mwaka jana.

Hata hivyo, Sheikh Ponda amesema kuwa, ZEC haikuwa na sababu ya kufuta uchaguzi  kwa kuwa, baada ya tume hiyo kutangaza matokeo, haina mamlaka ya kufuta.

Pamoja na kupinga kurudiwa kwa uchaguzi, Sheikh Ponda Sheikh Alhad amepata wapi kauli ya Kiongozi wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki), Sheikh Farid Hadi Ahmed kuwa anaunga mkutano marudio ya uchaguzi Zanzibar.

Sheikh Alhad kwenye mkutano wake jana alisema “Hata kiongozi wa Uamsho, Sheikh Farid Ahmad pia anaunga mkono suala la kufanyika uchaguzi wa marudio kwa mujibu wa barua yake aliyonitumia mimi .”

Sheikh Ponda ameeleza kwamba, Sheikh Farid hawezi kutoa kauli hiyo na kwamba kama Sheikh Alhad anayo barua hiyo, aitoe hadharani.

“Sio jambo rahisi kuamini kwamba Sheikh Farid anaweza kutoa kauli hiyo, sio jambo rahisi kabisa na kama ni kweli basi atoe ushahidi wake,”ameeleza Sheikh Ponda.

Pia Sheikh Ponda ameonesha kushangazwa na ZEC kuhalalisha matokeo ya Rais wa Muungano wa Tanzania sambamba na Wabunge wa Bunge la Muungano.

Shekh Ponda amesema kuwa uchaguzi wa Zanzibar na matokeo yake bado ni halali “Sisi kama Tasisi ya Waislamu tunapinga kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar.”

Amesema kuwa, taasisi hiyo imeunga mkono hatua za mwanzo zilizochukuliwa na CUF pia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kunusuru hali ya kisiasa visiwani humo na kutaka majadiliano yaendelee.

Shekh Ponda amemshauri Rais John Magufuli kutimiza ahadi yake aliyoitoa bungeni ya kushughulikia mzozo huo kwa kushirikiana na Maalim Seif Shariff Hamad na Dk. Ali Mohammed Shein.

Amesema kuwa, Rais Magufuli hajatoa tamko lolote na kwamba hajaeleza amefikia wapi katika kutatua mzozo huu.

Sheikh Ponda amesema kuwa kuna viashiria vya kuvunjika kwa amani visiwani humo kutokana na watu kuporwa haki zao na kwamba watakapoamua kuitafuata kutazuka vurugu.
Previous
Next Post »
My photo

Hi, I`m Sostenes, Electrical Technician and PLC`S Programmer.
Everyday I`m exploring the world of Electrical to find better solution for Automation. I believe everyday can become a Electrician with the right learning materials.
My goal with BLOG is to help you learn Electrical.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Label

KITAIFA NEWS KIMATAIFA MICHEZO BURUDANI SIASA TECHNICAL ARTICLES f HAPA KAZI TU. LEKULE TV EDITORIALS ARTICLES DC DIGITAL ROBOTICS SEMICONDUCTORS MAKALA GENERATOR GALLERY AC EXPERIMENTS MANUFACTURING-ENGINEERING MAGAZETI REFERENCE IOT FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY ELECTRONICS ELECTRICAL ENGINEER MEASUREMENT VIDEO ZANZIBAR YETU TRANSDUCER & SENSOR MITINDO ARDUINO RENEWABLE ENERGY AUTOMOBILE SYNCHRONOUS GENERATOR ELECTRICAL DISTRIBUTION CABLES DIGITAL ELECTRONICS AUTOMOTIVE PROTECTION SOLAR TEARDOWN DIODE AND CIRCUITS BASIC ELECTRICAL ELECTRONICS MOTOR SWITCHES CIRCUIT BREAKERS MICROCONTROLLER CIRCUITS THEORY PANEL BUILDING ELECTRONICS DEVICES MIRACLES SWITCHGEAR ANALOG MOBILE DEVICES CAMERA TECHNOLOGY GENERATION WEARABLES BATTERIES COMMUNICATION FREE CIRCUITS INDUSTRIAL AUTOMATION SPECIAL MACHINES ELECTRICAL SAFETY ENERGY EFFIDIENCY-BUILDING DRONE NUCLEAR ENERGY CONTROL SYSTEM FILTER`S SMATRPHONE BIOGAS POWER TANZIA BELT CONVEYOR MATERIAL HANDLING RELAY ELECTRICAL INSTRUMENTS PLC`S TRANSFORMER AC CIRCUITS CIRCUIT SCHEMATIC SYMBOLS DDISCRETE SEMICONDUCTOR CIRCUITS WIND POWER C.B DEVICES DC CIRCUITS DIODES AND RECTIFIERS FUSE SPECIAL TRANSFORMER THERMAL POWER PLANT cartoon CELL CHEMISTRY EARTHING SYSTEM ELECTRIC LAMP ENERGY SOURCE FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 2 BIPOLAR JUNCTION TRANSISTOR 555 TIMER CIRCUITS AUTOCAD C PROGRAMMING HYDRO POWER LOGIC GATES OPERATIONAL AMPLIFIER`S SOLID-STATE DEVICE THEORRY DEFECE & MILITARY FLUORESCENT LAMP HOME AUTOMATION INDUSTRIAL ROBOTICS ANDROID COMPUTER ELECTRICAL DRIVES GROUNDING SYSTEM BLUETOOTH CALCULUS REFERENCE DC METERING CIRCUITS DC NETWORK ANALYSIS ELECTRICAL SAFETY TIPS ELECTRICIAN SCHOOL ELECTRON TUBES FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 1 INDUCTION MACHINES INSULATIONS ALGEBRA REFERENCE HMI[Human Interface Machines] INDUCTION MOTOR KARNAUGH MAPPING USEUL EQUIATIONS AND CONVERSION FACTOR ANALOG INTEGRATED CIRCUITS BASIC CONCEPTS AND TEST EQUIPMENTS DIGITAL COMMUNICATION DIGITAL-ANALOG CONVERSION ELECTRICAL SOFTWARE GAS TURBINE ILLUMINATION OHM`S LAW POWER ELECTRONICS THYRISTOR USB AUDIO BOOLEAN ALGEBRA DIGITAL INTEGRATED CIRCUITS FUNDAMENTAL OF ELECTRICITY 3 PHYSICS OF CONDUCTORS AND INSULATORS SPECIAL MOTOR STEAM POWER PLANTS TESTING TRANSMISION LINE C-BISCUIT CAPACITORS COMBINATION LOGIC FUNCTION COMPLEX NUMBERS ELECTRICAL LAWS HMI[HUMANI INTERFACE MACHINES INVERTER LADDER DIAGRAM MULTIVIBRATORS RC AND L/R TIME CONSTANTS SCADA SERIES AND PARALLEL CIRCUITS USING THE SPICE CIRCUIT SIMULATION PROGRAM AMPLIFIERS AND ACTIVE DEVICES BASIC CONCEPTS OF ELECTRICITY CONDUCTOR AND INSULATORS TABLES CONDUITS FITTING AND SUPPORTS CONTROL MOTION ELECTRICAL INSTRUMENTATION SIGNALS ELECTRICAL TOOLS INDUCTORS LiDAR MAGNETISM AND ELECTROMAGNETISM PLYPHASE AC CIRCUITS RECLOSER SAFE LIVING WITH GAS AND LPG SAFETY CLOTHING STEPPER MOTOR SYNCHRONOUS MOTOR AC METRING CIRCUITS APPS & SOFTWARE BASIC AC THEORY BECOME AN ELECTRICIAN BINARY ARITHMETIC BUSHING DIGITAL STORAGE MEMROY ELECTRICIAN JOBS HEAT ENGINES HOME THEATER INPECTIONS LIGHT SABER MOSFET NUMERATION SYSTEM POWER FACTORS REACTANCE AND IMPEDANCE INDUCTIVE RESONANCE SCIENTIFIC NOTATION AND METRIC PREFIXES SULFURIC ACID TROUBLESHOOTING TROUBLESHOOTING-THEORY & PRACTICE 12C BUS APPLE BATTERIES AND POWER SYSTEMS ELECTROMECHANICAL RELAYS ENERGY EFFICIENCY-LIGHT INDUSTRIAL SAFETY EQUIPMENTS MEGGER MXED-FREQUENCY AC SIGNALS PRINCIPLE OF DIGITAL COMPUTING QUESTIONS REACTANCE AND IMPEDANCE-CAPATIVE RECTIFIER AND CONVERTERS SEQUENTIAL CIRCUITS SERRIES-PARALLEL COMBINATION CIRCUITS SHIFT REGISTERS BUILDING SERVICES COMPRESSOR CRANES DC MOTOR DRIVES DIVIDER CIRCUIT AND KIRCHHOFF`S LAW ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS 1 ELECTRICAL DISTRIBUTION EQUIPMENTS B ELECTRICAL TOOL KIT ELECTRICIAN JOB DESCRIPTION LAPTOP THERMOCOUPLE TRIGONOMENTRY REFERENCE UART WIRELESS BIOMASS CONTACTOR ELECTRIC ILLUMINATION ELECTRICAL SAFETY TRAINING FILTER DESIGN HARDWARE INDUSTRIAL DRIVES JUNCTION FIELD-EFFECT TRANSISTORS NASA NUCLEAR POWER SCIENCE VALVE WWE oscilloscope 3D TECHNOLOGIES COLOR CODES ELECTRIC TRACTION FEATURED FLEXIBLE ELECTRONICS FLUKE GEARMOTORS INTRODUCTION LASSER MATERIAL PID PUMP SEAL ELECTRICIAN CAREER ELECTRICITY SUPPLY AND DISTRIBUTION MUSIC NEUTRAL PERIODIC TABLES OF THE ELEMENTS POLYPHASE AC CIRCUITS PROJECTS REATORS SATELLITE STAR DELTA VIBRATION WATERPROOF