WAZIRI
Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye aliyekuwa amelazwa katika Taasisi ya
Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyoko Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH), ameruhusiwa kurudi nyumbani.
Ofisa
Uhusiano Msaidizi wa MNH, John Steven, jana alisema Sumaye aliruhusiwa
juzi jioni baada ya madaktari kuridhishwa na maendeleo ya afya yake.
“Sumaye
amepewa ruhusa ya kurudi nyumbani tangu juzi jioni, madaktari wake
waliridhishwa na mwenendo wa afya yake kutokana na matibabu waliyompatia
dhidi ya ugonjwa uliokuwa unamsumbua,” alisema.
Hata
hivyo, Steven hakufafanua ugonjwa uliokuwa ukimsumbua kiongozi huyo
mstaafu kwa kile alichoeleza kuwa kanuni na sheria za kitabibu
zinakataza.
“Siwezi kutaja ugonjwa uliomfanya akalazwa hapa, mwenyewe anaweza kuwaeleza kwa sababu ni siri yake na daktari wake,” alisema.
Sumaye
alilazwa hospitalini hapo Januari 7, mwaka huu na Januari 11, Rais John
Magufuli, alimtembelea hospitalini hapo na kumpa pole.
Mapema
mwaka huu, Sumaye alitangaza rasmi kujiunga na Chadema baada ya
kuondoka katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka jana muda mfupi kabla ya
kampeni za uchaguzi.
No comments:
Post a Comment