Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akifanya mazungumzo na Balozi wa Qatar
Mhe. Abdullah Jassim Almaadadi alipofika Wizarani kwa ajili ya
kumpongeza kwa kuteuliwa katika wadhifa wake mpya na pia kumhakikishia
ushirikiano kati ya Tanzania na Qatar. Mazungumzo hayo yalifanyika
tarehe 30 Desemba, 2015.
Balozi Al maadadi naye akizungumza huku Mhe. Mahiga akimsikiliza.
.......Mkutano na Balozi wa Kuwait nchini
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda
na Kimataifa, Mhe. Augustine Mahiga (kulia) akizungumza na Balozi wa
Kuwait nchini Mhe. Nassem Ibrahim Al Najib, alipokuja kumtembelea
Wizarani na kufanya mazungumzo naye kuhusu namna ya kuimarisha
ushirikiano kati ya Tanzania na Kuwait na pia kumpongeza.
Balozi Mahiga akiagana na Balozi wa Kuwait mara baada ya kumaliza mazungumzo naye.
No comments:
Post a Comment