Serikali Yazifunga Redio 28 Kwa Kushindwa Kulipa Ada ya Leseni - LEKULE BLOG

Breaking

Header Ads

Saturday, 16 January 2016

Serikali Yazifunga Redio 28 Kwa Kushindwa Kulipa Ada ya Leseni


Serikali imezifungia redio 28  kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo  kushindwa kulipa ada za leseni na kutimiza masharti yaliyowekwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Professa Makame Mbarawa, alisema majina ya redio zilizofungwa yatatangazwa baadaye na TCRA.


“Natoa agizo kwa kampuni mbalimbali kulipa ada za leseni kwa wakati ambao umepangwa na TCRA na ambao hawatatekeleza agizo hilo watachukuliwa hatua za kisheria,” alisema Profesa Mbarawa.
Post a Comment