Rais
John Magufuli anatarajiwa kuwasili mkoani hapa leo kwa ziara ya kikazi
ya siku mbili. Hii ni ziara yake ya kwanza tangu alipoapishwa kushika
wadhifa huo Oktoba 25, mwaka jana.
Maandalizi
ya kumpokea Rais yalikuwa yamepamba moto jana ikiwa ni pamoja na
kupanua barabara inayoingia na kutoka makazi ya Rais jijini hapa.
Katika
Ikulu ndogo ya jijini Arusha jana jioni, wafanyakazi walionekana
wakiweka mazingira sawa ya kumpokea Rais ambaye atawasili mchana kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia).
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumlaki kiongozi huyo.
“Tuonyeshe
moyo wa upendo na ukarimu kwani mkoa huu una heshima ya kuwapokea
viongozi wa kitaifa na kimataifa na ulinzi umeimarishwa kuhakikisha muda
wote kunakuwa salama,” alisema Ntibenda.
Mkuu
wa Wilaya ya Arusha Mjini, Fadhili Nkurlu alikagua barabara inayoelekea
Ikulu ndogo huku askari polisi wakiwa doria katika barabara zinazoingia
na kutoka eneo hilo.
Katika
ziara hiyo, Rais Magufuli ambaye pia Amiri Jeshi Mkuu, atatembelea Chuo
cha Jeshi cha TMA, Monduli ambako keshokutwa, atawatunuku kamisheni ya
uofisa, maofisa wateule wa jeshi.
Iwapo
Rais Magufuli atafikia Ikulu ndogo ambayo makazi ya kiongozi wa nchi
anapokuwa kwenye ziara mikoani, atakuwa anatendea kazi kauli zake wakati
wa kampeni za kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.
No comments:
Post a Comment