RAIS
John Magufuli ametoa mwito kwa Watanzania kumuombea ili aendelee
kuwashughulikia wote wanaofanya ubadhirifu wa fedha za umma kupitia
kampeni yake ya kutumbua majipu.
“Nataka
niwahakikishieni kuwa nitaendelea kutumbua majipu yote mpaka yaishe, na
naomba mniombee ili kazi hii ya kutumbua majipu ifanyike kwa
mafanikio,” alisema Dk Magufuli.
Alitoa
kauli hiyo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi katika mikoa ya
Kilimanjaro na Arusha jana, alipotua kwa ziara ya kikazi ikiwa ni ya
kwanza kwao tangu achaguliwe kushika wadhifa huo Novemba 5, mwaka jana.
Dk
Magufuli aliwasili mkoani Arusha, ambako kesho atatunuku Kamisheni kwa
maofisa wanafunzi wa kundi la 57/15 katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi
(TMA) Monduli mkoani hapa.
Rais
Magufuli aliwasili mjini Arusha akitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Kilimanjaro (KIA), alikotua kwa ndege akitokea jijini Dar es Salaam
na kupokewa na mamia ya wananchi.
Akiwa
uwanjani hapo, Rais Magufuli aliwashukuru wananchi kwa mapokezi makubwa
aliyoyapata na aliwaeleza kuwa uchaguzi umekwisha, kilichobaki ni kazi
tu.
“Nawashukuru
sana ndugu wananchi kwa mapokezi haya makubwa, naomba kuwahakikishia
kuwa uchaguzi umekwisha na sasa kilichobaki ni kuchapa kazi tu,” alisema Rais Magufuli.
Alisema
yote aliyoyaahidi kwa wananchi wa mkoa wa Arusha na Watanzania kwa
ujumla, ikiwemo ujenzi wa barabara za Arusha, kulipa fidia za wananchi
na kufuta ada ya shule za msingi na sekondari yanatekelezwa.
Rais
Magufuli alisisitiza kuwa serikali yake haitawabagua Watanzania kwa
dini zao wala makabila yao na wala haitawabagua kwa misingi ya vyama
vyao na kanda zao.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwasili
kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa KIA mkoani Kilimanjaro jana huku
akiongozana na Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda
tayari kwa hafla ya kuwatunuku kamisheni maafisa wapya wa jeshi la
Wananchi waliohitimu vyema mafunzo yao katika chuo cha Jeshi Monduli
Mkoani Arusha itakayofanyika Januari 23 /2016. PICHA NA IKULU
Rais
wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akishiriki
kupiga ngoma za utamaduni wakati alipowasili kwenye uwa nja wa ndege wa
KIA mkoani Kilimanjaro jana
Rais
wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana
na wananchi waliofika kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa KIA mkoani
Kilimanjaro.
Baadhi
ya wananchi wakimpungia mikono Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Dk. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa
kimataifa wa KIA mkoani Klimajaro.
No comments:
Post a Comment