Jenerali Godefroid Niyombare aliyeongoza jaribio la mapinduzi ya kijeshi yaliotibuliwa, Mei 13 hadi jioni
Na RFI
Kundi
jipya la waasi nchini Burundi FOREBU lililoundwa hivi karibuni kwa
minajili ya kumtimua madarakani Rais Pierre Nkurunziza, limetangaza
kumteua Alhamisi hii Januari 21 jenerali Godefroid Niyombare kuliongoza
kundi hilo.
Jenerali Godefroid Niyombare aliongoza mapinduzi ya kijeshi yaliyotibuliwa jioni ya tarehe 13 Mei mwaka 2015 nchini Burundi.
Jenerali
Nyombare, mwenye umri wa miaka 47, alikuwa mshirika wa karibu wa Pierre
Nkurunziza, kiongozi wa zamani wa kundi la waasi wa kihutu CNDD-FDD
(1993-2006) wakati wa vita vya maguguni vilivyokua vikiendeshwa na kundi
hilo dhidi ya majeshi ya Burundi.
Jenerali
Niyombare alikua kiongozi wa kwanza wa majeshi ya Burundi kutoka kabila
la Wahutu (2009-2013), kisha mkuu wa idara ya taifa ya Ujasusi (SNR)
kati ya mwezi Desemba 2014 na mwezi Machi 2015 alipofutwa kazi. "Uratibu
wa kundi la waasi la FOREBU unasimamiwa na jenerali Godefroid
Niyombare", msemaji mpya wa kundi hilo jenerali Edouard Niragira
ametangaza ambapo sauti yake iliyorekodiwa imetumwa kwenye ofisi ya
shirika la habari la Ufaransa AFP.
Jenerali
Edouard Nibigira, afisa mwandamizi wa cheo cha juu katika polisi aliwahi
kuhudumu kama mkurugenzi wa polisi inayopambana na Majanga.
Jenerali
Niyombare tangu mwezi Novemba anakabiliwa na vikwazo vya Marekani,
pamoja na kiongozi namba mbili wa mapinduzi Cyrille Ndayirukiye
aliyekamatwa na kuhukumiwa hivi karibuni kifungo cha maisha jela.
Kanali
Jules Ndihokubwayo, kutoka kundi la zamani la waasi la CNDD-FDD, ambaye
aliwahi kuhudumu katika kitengo cha mawasiliano katika kikosi cha
wanajeshi wa Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) na ambaye hivi
karibuni alilitoroka jeshi la Burundi, ameteuliwa kuwa mkuu wa majeshi
ya kundi la waasi la FOREBU. Anashirikiana na Luteni Kanali Edouard
Nshimirimana, mpaka sasa msemaji wa kundi hili jipya la waasi, ambaye
amethibitisha kwa AFP taasisi hizo mpya zakundi hilo.
Burundi
imetumbukia katika mgogoro mkubwa wenye machafuko tangu mwezi Aprili,
kufuatia uamuzi wa Pierre Nkurunziza wa kutangaza kuwania muhula wa tatu
kwenye kiti cha urais. Uamuzi ambao kwa mujibu wa wapinzani wake,
unaukiuka Katiba na Mkataba wa Amani na Maridhiano wa Arusha uliomaliza
vita vilivyodumu zaidi ya mwongo mmoja kati ya makundi ya waasi na
jeshi, ambalo wakati huo lilikua likiundwa na idadi kubwa ya Watutsi na
makundi ya waasi yaliokua yakiundwa na Wahutu.
Kundi
hili jipya la waasi linatafuta kuunganisha makundi yote ya waasi ili
waweze kumn'goa madarakani Rais Pierre Nkurunziza, afisa wa FOREBU,
ambaye hakutaka jina lake litajwe ameliambia shirika la habari la
Ufaransa AFP. "Sio mshangao kuona tangazo hili linatolewa sanjari na
kuwasili kwa (ujumbe) wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini
Bujumbura", ameongeza afisa huyo.
Upande wa serikali hawajazungumzia chochote kuhusu tangazo hili.
Hayo
yakijiri hali ya wasiwasi inaendelea kutanda katika maeneo mbalimbali
nchini Burundi, hasa mjini Bujumbura, ambapo polisi imeendelea na
operesheni yake ya kamata kamata, huku vijana wakilengwa zaidi.
No comments:
Post a Comment