DAR ES SALAAM: Zikiwa zimepita
siku chache tangu staa wa filamu, Wastara Juma kufunga ndoa na Mbunge wa
Jimbo la Donge, Zanzibar, Sadifa Juma aliyekuwa mpenzi wake, Bond
Suleiman nusu afe, Risasi Mchanganyiko lina mkanda kamili.
Wastara na Bond
Wakizungumza na gazeti hili, ndugu wa
karibu wa kijana huyo ambaye pia ni muigizaji (jina linahifadhiwa)
alisema siku moja kabla ya ndoa ya Wastara, Bond alitaka kujiua kwa
kunywa sumu, lakini kaka yake aliyeingia chumbani kwake ghafla,
akamuwahi kabla hajaibugia.
Bond
“Ni Mungu tu Bond kuwa hai mpaka sasa,
japokuwa hayupo vizuri ni kama amepaniki kutokana na Wastara kuolewa,
maana bado anampenda, ungekuta sasa hivi tunaongea mengine, kwani
alikuwa ameshaweka sumu tayari anywe, lakini alisahau kufunga mlango
ikawa ndiyo salama yake baada ya kaka yake kuingia chumbani kwake akiwa
anahitaji kuzungumza naye ndipo akakutana na ishu hiyo na kufanikiwa
kumuokoa.
“Ukweli hata sisi tumeumia sana Wastara
kuolewa na mtu mwingine kwani tulikuwa tukimfahamu kwamba atakuja
kufunga ndoa na Bond maana aliwahi kuletwa kutambulishwa kwa ndugu,”
alisema ndugu huyo.
Gazeti hili lilimtafuta Bond ili kupata
ukweli wa habari hizo, ambapo alikiri kuokolewa na kaka yake baada ya
kutaka kunywa sumu kutokana na Wastara kuolewa.
“Nilikuwa nimeshaandaa sumu kabisa na
Wastara nilimuaga kwa njia ya meseji na hii ni baada ya kuniambia siku
inayofuata anaolewa, ukweli nilimpenda na najuta maana mimi ndiyo
nilifanya makosa na kumkosea sana, lakini siku niliyoamua kuachana na
mambo ya ufuska na kuwa mtu wa sala muda wote, naye naona ndiyo akasema
basi hanitaki tena.
“Nilijitahidi sana kumuomba msamaha
lakini akanikatalia na kusema amempata atakayempa faraja ya moyo,
namtakia maisha mema ya ndoa na nitamsubiri kama ndoa itavunjika
nitamuoa maana mwenyewe wakati anasubiri kufunga ndoa (Alhamisi
iliyopita) aliniambia kwamba anaogopa ndoa hiyo,” alisema.
No comments:
Post a Comment