Ronaldo akionesha mkoko wake mpya wa bei chafu aina ya Porsche Turbo SMara baada ya kukosa tuzo ya mchezaji bora wa dunia (Ballon d’Or)
iliyochukuliwa na mpinzani wake wa muda mrefu Lionel Messi, mshambuliaji
wa Real Madrid na nahodha wa Ureno alionekana katika morali ya juu
kabisa mara baada ya kupost picha katika mtandao wake wa Instagram akiwa
ameketi na gari mpya aina ya Porsche Turbo S yenye thamani ya dola
146,000 za Marekani.
Ronaldo mwenye miaka 30 hivi sasa, alikosa tuzo hiyo ambayo ingekua
ni ya nne kwake kama angetwaa laikini aliishuhudia ikienda kwa Lionel
Messi wa Barcelona na kumfanya muargentina huyo kufikisha tuzo 5 tangu
alipochukua 2009, 2010, 2011, 2012 na 2015. Ronaldo
amekosa tuzo ya Ballorn d’Or ambayo ilinyakuliwa na Messi endapo
Ronaldo angetwaa tuzo hiyo, ingekuwa ni mara yake ya nne kuichukukuaPamoja na Ronaldo kutokuchukua tuzo hiyo lakini ndiye aliyekua
mfungaji bora wa mabao katika michuano yote msimu uliopita ingawa
hakufanikiwa kuisaidia Real Madrid kutwaa taji lolote wakati Messi
aliisaidia Barcelona kushinda mataji yote waliyoshiriki. Lionel Messi akiwa na tuzo yake ya Ballon d’Or ya tano alitwaa siku chache zilizopita kwa kuwashinda Cristiano Ronaldo na NeymarAkiongea na mtandao wa klabu yake ya Madrid, Cristiano amesema kuwa,
siku zote hawezi kuacha kufurahisha mashabiki wake na wote wanaomsapoti
huku akisisitiza kuwa atazidi kujituma kuisaidia Madrid kutwaa mataji,
kufunga magoli mengi kila msimu, sanjari na kuwa sehemu ya timu (team
player). Sergio Ramos, Marcelo, Luka Modric na Ronaldo katika pose na uzo zao kikosi bora cha mwaka cha FIFA (FIFPro XI awards)
Ronaldo ambaye ndiye kinara wa mabao katika historia ya klabu ya Real
Madrid hivi sasa mara baada ya kuvunja rekodi iliyokua inashikiriwa na
legendari Raul Gonzalez, amesema ataendelea kufunga magoli na kuweka
rekodi mpya ikiwemo kufikisha hata magoli 1000.
No comments:
Post a Comment