DAR ES SALAAM: Habari
zinazosambaa kwa kasi ya ajabu kama moto wa kifuu zinaeleza kuwa, mtoto
mzuri ndani ya Bongo Movies, Wema Sepetu ‘Madam’ mbali na taarifa za
kuwa mjamzito, hadi sasa bado yupo kwenye wakati mgumu kuweza kutegua
kitendawili cha nani mmiliki halali wa kiumbe kilichopo tumboni mwake,
Risasi Mchanganyiko linakupa habari kamili.
Hivi karibuni, magazeti tofauti ya
Global Publishers ndiyo yalikuwa ya kwanza kuripoti kuhusu uwepo wa
mimba ya mlimbwende huyo asiyechuja Bongo, ambapo awali, vyanzo
mbalimbali vilieleza kuwa mhusika ni mbunge mmoja machachari ambaye
ndiye anayemuweka Wema mjini kwa sasa.
Kitumbo cha Wema Sepetu
MAJIBU YA WEMA ALIPOBANWA
Kwenye habari ya awali iliyoripotiwa na
gazeti la Ijumaa, Wema alipotafutwa kusomewa mashitaka yake kuwa ana
ujauzito wa mbunge huyo, kupitia simu ya shosti wake, Aunt Ezekiel, staa
huyo hakutaka kufunguka sana kuhusu mbunge huyo zaidi ya kusema; “ndiyo
nina mimba, tena ya miezi sita.”
UBUYU MPYA SASA
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Miss
Tanzania huyo wa mwaka 2006 amejiridhisha kuwa ni mjamzito baada ya
kupima kwenye hospitali moja maarufu (jina tunalo) na kuondoka na furaha
ya ajabu lakini kitendawili alichoondoka nacho ni kuwa hamjui mhusika
wa kiumbe hicho.
WOTE AWAPA ASILIMIA 50
“Madam alifurahi kweli maana suala
lililokuwa linamnyima usingizi siku zote ni kutopata mimba. Baada ya
furaha hiyo, ishu ikawa ni kumtambua mhusika kwani kwa nyakati tofauti
ameshabanjuka kimalavidavi na mshindi wa Big Brother Hot Shot 2014,
Idris Sultan na mbunge yule anayempa jeuri ya pesa kwa sasa, wote
amewapa asilimia hamsini hajajua nani hasa ndiyo mhusika,” kilisema
chanzo hicho.
WOTE WAWILI KAWAMILIKISHA
Chanzo hicho kilizidi kutiririka kuwa,
baada ya kuona ameshachanganya madawa, Madam aliamua kila mmoja
kumwambia kuwa ‘mzigo’ huo ni wake hivyo wote kwa pamoja na nyakati
tofauti wanahudumia na kumjali staa huyo, tena kwa nguvu zote.
“Yaani kila mmoja kamwambia mimba yake.
Wote wawili wamezipokea taarifa za ujauzito kwa bashasha huku kila mmoja
akijiamini kuwa ni mhusika pasipo kujua Madam hajui nani hasa ndiye
halisi.
MBUNGE, IDRISS ‘FULL’ KUHUDUMIA
“Yani ni full kuhudumia. Mbunge kwa
wakati wake amekuwa akimwaga chapaa kama hana akili nzuri. Amelipia
nyumba ile ya Ununio jijini Dar na kama hiyo haitoshi, amekuwa
akisimamia shopping za maana tu mjini na hata ile ndiga aliyojizawadia
Wema katika sherehe yake ya kuzaliwa, mbunge huyo alihusika katika
malipo,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Idris naye si haba. Anajitutumua kwa upande wake, anaamini kwamba mzigo ni wake bila kujua mimba hiyo ina figisufigisu.”
IDRIS ASAKWA, AFUNGUKA
Gazeti hili lilimtafuta Idris kupitia simu yake ya mkononi ambapo alipopokea, alitiririka hivi:
Risasi: Mzee tumepata habari kwamba wewe ndiyo mhusika wa mimba ya Madam, vipi unazungumziaje taarifa hizo?
Idris: Kwenye hilo kwa sasa siwezi kuliongelea, labda unipe mwezi mmoja. Kichwa changu hakijatulia.
Risasi: Lakini inasemekana unagharamia kila kitu kwa sasa, ukiamini mzigo ni wako?
Idris: Aaa! Acha kuniingizia hayo mambo bwana. Wewe subiri huo mwezi mmoja ukipita nitakueleza kila kitu.
SHOGA ZAKE WAMSHANGAA!
Mashosti wake waliozungumza na Gazeti
hili ambao hawakutaka kutajwa majina yao, walisema ni jambo la
kushangaza kwa mwanamke kushindwa kumjua mwanaume aliyempa ujauzito.
WEMA ANASEMAJE?
Gazeti hili lilifanya jitihada za
kutosha kumsaka Wema kwa kumpigia simu na kumtumia ujumbe mfupi lakini
hakupokea wala kujibu ujumbe huo.
KUTOKA KWA MHARIRI
Mimba ni jambo la kheri hivyo kwa kuwa
Wema ameziona simu za wanahabari wetu zikimuuliza juu ya mhusika wa
kiumbe hicho, ni vyema akawapigia na kuanika kila kitu kuhusu habari
hii.
No comments:
Post a Comment