Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb.) akisalimiana na Balozi wa
Kuwait hapa nchini, Mhe. Nassem Ibrahim Al Najib alipofika Wizarani kwa
ajili ya kuwasilisha salamu za pongezi kwa Mhe. Dkt. Kolimba kutoka kwa
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait.
Mhe. Balozi Al Najib akimkabidhi Mhe. Dkt. Kolimba salamu za pongezi kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait.
Mhe.
Dkt. Kolimba nae akimshukuru Balozi Al Najib kwa kuwasilisha salamu hizo
za pongezi na kwamba amezipokea na kuahidi kuwa Tanzania itaendelea
kushirikiana na Kuwait katika masuala mbalimbali ya maendeleo.
Sehemu
ya ujumbe kutoka Wizarani wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Dkt.
Kolimba na Balozi wa Kuwait hapa nchini (hawapo pichani). Kutoka kushoto
ni Bw. Batholomeo Jungu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya
Kati, Bw. Tahir Bakari, Afisa Mambo ya Nje na Bw. Adam Isara, Msaidizi
wa Naibu Waziri.
No comments:
Post a Comment