Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipata maelezo
ya uboreshaji unaoendelea kufanyika wa kiwanja cha Ndege Terminal Two
kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),
Eng. Suleiman Suleiman jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa TAA Eng. Suleiman Suleiman akimwonyesha Waziri Prof. Mbarawa ujenzi
unaoendelea wa jengo la tatu la abiria (Terminal three), ambapo jengo
hilo likikamilika litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 6 kwa
mwaka.
Mkurugenzi
wa TAA Eng. Suleiman Suleiman akimwonyesha Prof. Makame Mbarawa eneo
ambalo limefanyiwa ukarabati kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere
International Airport (JNIA), wakati alipotembelea eneo hilo, jijini Dar
es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na
wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA), na kuagiza
Mamlaka hiyo kuongeza mapato ili kuweza kupanua fursa za uwekezaji na
kuendeleza uchumi wa nchi.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametembelea
Mamlaka ya Viwanja vya ndege (TAA) na Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini
(TCAA) jijini Dar es salaam na kuagiza Mamlaka hizo kuboresha huduma na
kuongeza mapato ili kupanua fursa za uwekezaji na kukuza uchumi wa
nchi.
Waziri
Mbarawa amesisitiza kuwa mapato yatakayokusanywa yawe yanatoka kwa
makampuni ambayo yapo chini ya mamlaka hizo na si kwa kuwabana wananchi.
‘Nataka
msiongeze mapato kwa kuwaathiri wananchi na badala yake mtafute vyanzo
vingine vya mapato ambavyo vitasaidia katika kuchochea fursa za
uwekezaji’, amesema Waziri Mbarawa.
Aidha,
Profesa Mbarawa ametaka huduma zote katika viwanja vya ndege kama zima
moto,uhamiaji,polisi na huduma za afya, ziwe chini ya mamlaka ya viwanja
vya ndege ili kurahisisha uharaka na ukaribu wa huduma kumfikia mteja
kwa urahisi.
‘Ninyi
ndio kioo cha jamii, hivyo basi haipaswi kuchukua zaidi ya dakika kumi
kumhudumia mteja mmoja au kuwa na tabia ya kumsumbua mteja pindi
anapohitaji huduma’, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Ameitaka
TAA kufanya utaratibu wa kujenga jengo kubwa la ofisi kwa ajili yao na
kukodisha kwani kufanya hivyo kutaongeza mapato katika Mamlaka hiyo.
Awali
wakati akitoa taarifa kwa Waziri Mbarawa Mkurugenzi wa TAA Eng. Suleiman
Suleiman amesema kuwa Mamlaka hiyo imeweza kuhakikisha kuwa huduma za
usafirishaji kama za ufundi na zimamoto na uokoaji zinaridhisha.
Katika
hatua nyingine wakati akiwa katika Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania
(TCAA), kuwa waadilifu na kufanya kazi kwa uharaka katika uendaji kazi
wao ili kuendana na kasi ya mabadiliko anayoitaka Rais John Pombe
Magufuli
“Najua
ni waadilifu katika kazi zenu ila nawaomba muongeze, pasiwe na usumbufu
kila mtu ana haki ya kupata huduma stahiki anayohitaji na kwa wakati
unaotakiwa” amesisitiza Waziri Mbarawa.
Ameitaka TCAA kujitathmini wao binafsi, wateja na huduma wanazozitoa kwa wateja wao ili kuhakikisha sekta yao inakuwa.
Naye
Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Charles Chacha ameitaja baadhi
ya miradi inayotekelezwa na Mamlaka hiyo kuwa ni uwekaji wa mitambo ya
kisasa ya kuongoezea ndege na kufuatilia safari za ndege nchini iitwayo
‘Automatic Dependent Surveillance’.
Ameainisha
kuwa mradi mwingine ni ununuzi wa rada mbili za kuongozea ndege za
kiraia ambazo zitafungwa katika viwanja vya Julius Nyerere (JNIA) jijini
Dar es salaam na KIA mkoani Kilimanjaro.
IMETOLEWA NA
KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO
WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.
No comments:
Post a Comment