Serikali
imepiga marufuku tabia ya baadhi ya hospitali au taasisi binafsi za
afya kuwapima wagonjwa wanaotoka hospitali za Serikali vipimo ambavyo
hawakuagizwa kuvipima na madaktari kutoka hospitali hizo kwani kufanya
hivyo ni kuiongezea Serikali gharama zisizo la lazima.
Tamko
hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangala wakati alipofanya ziara ya
kutembelea leo kwenye Taasisi ya Saratani ya Ocean Road iliyopo jijini
Dares Salaam.
Waziri
Kingwangala alitoa agizo hilo baada ya kukutana na mgonjwa ambaye
alitakiwa kufanya kipimo cha MRI katika hospitali moja ya binafsi
jijini Dar es Salaam, lakini hospitali hiyo ilimpima mgonjwa huyo vipimo
vingine ambayo havikupaswa kupimwa.
Alisema
fedha zilizotumika kulipia vipimo hivyo vya ziada vingetumika kununulia
dawa na vifaa tiba ambavyo vingetumika kuwahudumia wananchi wengi
zaidi.
Aidha
Naibu Waziri huyo aliwataka watendaji wa afya kutumia utaalamu na
ujuzi wao kuaanda mipango ya kuweza kukabaliana na changamoto za sekta
ya afya nchini.
“Ni
lazima tutumia utaalamu tulioupata katika kupunguza shida za watu
katika sekta ya afya. Tumumie elimu tuliyoipata shuleni na vyuoni ili
kuboresha maisha ya Watanzania na tumsaidie Rais John Pombe Mafuguli
tusisubiri hadi tuambiwe tufanye nini,”alisisitiza.
Mgonjwa huyo matibabu yake yanalipiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Kitendo
cha hospitali hiyo kilionesha kumsikitisha Naibu Waziri huyo kwa kuwa
fedha za Serikali ndizo zinazotumika kugharamia vipimo ambavyo, taasisi
hiyo haikumwandikia mgonjwa huyo.
“
Hospitali hii imetumia nafasi hiyo ya kupima mgonjwa huyo vipimo ambayo
hakuandikiwa na daktari aliyemwona katika taasisi hii. Chakushangaza
baadhi ya vipimo ambayo amepimwa vipo katika taasisi hiyo. Hospitali hii
imetumia vibaya mfumo wa mfuko huo kwa kumpima mgonjwa huyo vipimo vya
ziada,"alisema Naibu Waziri Kigwangala.
Aliwataka
watendaji wa afya kuhakikisha wanawapeleka wagonjwa wanaotakiwa kupimwa
vipimo vya MRI na CT- Scan katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH)
kwa kuwa hospitali hiyo ina vifaa vya kisasa na vinafanya kazi vizuri
kwa gharama nafuu.
Naibu Waziri huyo aliagiza uongozi huo kusitisha malipo ya vipimo hivyo vya ziada kwa kushirikiana na mfumo huo wa NHIF.
“Sitisheni
malipo ya vipimo vya ziada katika hospitali hiyo, mgonjwa ni wa taasisi
hii anaingiliwa na taasisi nyingine kwa kupimwa vipimo vingine ambavyo
havikupaswa kupimwa, hivi ni vijipu vidoovidogo vinatumbuliwa hapahapa,”
alisema Waziri huyo.
Katika
ziara hiyo Naibu Waziri huyo alielezwa kwamba taasisi hiyo inakabiliwa
na changamoto ya vipimo vya ugunduzi wa saratani na tiba ya satarani,
dawa, ambapo alisema atashirikiana na uongozi ili kuweza kukabiliana na
matatizo hayo.
Pia
aliutaka uongozi wa taasisi hiyo na watendaji wa afya pamoja na wizara
kufanya kazi kama timu ili kuweza kutatua changamoto zilizopo.
No comments:
Post a Comment