Msajili
wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali anakusudia kuyachukulia hatua
Mashirika yanayoendesha shughuli zao kinyume cha Sheria ya NGOs Na. 24
ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa mwaka 2005.
Mashirika
hayo ni yale ambayo hayajawasilisha taarifa za mwaka kwa kipindi cha
miaka miwili pasipo kutoa sababu za msingi, kulipa ada ya mwaka au
kuendesha shughuli za NGOs bila kusajiliwa chini ya Sheria ya NGOs.
Kwa
taarifa hii, Mashirika husika yanatakiwa yawe yamerekebisha dosari
tajwa ndani ya siku thelathini (30) kuanzia tarehe ya tangazo hili.
Baada
ya kipindi hicho, Msajili wa NGOs atayafutia usajili Mashirika ambayo
yatakuwa hayajawasilisha taarifa na kuyachukulia hatua stahiki Mashirika
yanayoendesha shughuli za NGOs bila ya usajili chini ya Sheria husika.
Malipo
yote ya ada yafanyike kupitia Benki ya NMB, NGO Account Na. 20110014074
na stakabadhi halali ya malipo itumwe kwa Msajili wa NGOs.
Imetolewa na:
M.S. Katemba
MSAJILI WA NGOs
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,
JINSIA, WAZEE NA WATOTO
06 Januari, 2015
No comments:
Post a Comment