Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe ameilalamikia serikali ya Magufuli kwa kitendo chake cha kukaa kimya kuhusu ufisadi unaoendelea kufanywa na Harbinder Singh Seth, mmiliki wa IPTL ambaye huvuna kiasi cha malipo ya bilioni 4 kila mwezi kama malipo ya kuliuzia umeme shirika la ugavi wa umeme nchini, Tanesco.
Zitto
ambaye ni mmoja wa wabunge walioibua na kusimamia kidete sakata la
ufisadi wa Tegeta Escrow bungeni mwishoni mwa mwaka juzi (2014), amesema
hayo kufuatia tangazo la serikali kuhusu kashfa ya Commodity Import
Support ya miaka ya miaka 1980 na 1990s, ambapo ameisifu serikali kwa
hatua hiyo na kuhoji iweje ikomae na kashfa hiyo tu, huku ikisita
kuchukua hatua kwenye sakata la IPTL linaloigharimu serikali kiasi
kikubwa cha fedha kila mwezi isivyostahili?
Kampuni
ya IPTL imeshalipwa fedha mara mbili tangu Rais Magufuli aingie rasmi
madarakani, hivyo kufanya hesabu zitimie bilioni 8 kwa kipindi cha miezi
miwili mpaka sasa.
==>Huu ndo ujumbe wa Zitto Kabwe aliouandika kupitia ukurasa wake wa facebook
"Nimeona
tangazo la Serikali kuhusu kashfa ya Commodity Import Support. Hii ni
kashfa ya miaka ya 1980s na 1990s. Ni hatua nzuri.
"Lakini
ina maana gani wakati Serikali inavuta miguu kwenye suala la IPTL?
Harbinder Singh Seth na genge lake wanavuta tshs 4bn kila mwezi.
"Kwa kutochukua hatua kuhusu IPTL, Rais Magufuli ameshaipotezea nchi mapato ya tshs 8bn tangu aingie madarakani. #TegetaEscrow ndio baba la mtandao wa ufisadi nchini kwetu" - Zitto Kabwe.
No comments:
Post a Comment