Rais Abdel Fattah el-Sissi wa Misri akilihutubia taifa
Wamisri
wanaadhimisha miaka mitano tangu lilipopiga wimbi la vuguvugu la
maandamano ya umma lililomng'oa madarakani mtawala wa muda mrefu Hosni
Mubarak.
Katika
hotuba yake aliyoitoa kwa njia ya Televisheni katika mkesha wa kuamkia
maadhimisho hayo Rais wa sasa wa nchi hiyo, Abdel- Fattah el-Sissi
alilipongeza vuguvugu lililouondoa utawala huo wa muda mrefu mwaka 2011
na kusema kuwa waandamanaji waliouawa wakati huo walikuwa wakipigania
kurejesha misingi halali na kujenga Misri mpya.
Maadhimisho
hayo yanakuja mnamo wakati ulinzi ukiwa umeimarishwa kwa kiwango cha
juu katika mji mkuu wa nchi hiyo Cairo kama tahadhari ya kuzuia
maandamano au mashambulizi yatakayovuruga sherehe hizo.
El-Sissi
ambaye alishinda uchaguzi wa mwaka 2014 kwa kishindo alilipongeza jeshi
la polisi nchini humo na kuahidi kuchukua hatua kali dhidi ya jambo
llolote litakaloonekana kitisho dhidi ya utulivu wa nchi hiyo.
Jeshi la Polisi lakosolewa kwa kukiuka misingi ya haki za binaadam
Pongezi
hizo kwa jeshi la polisi zinakuja huku kukiwa na malalamiko kadhaa
kutoka kwa wanaharakati wa haki za binadamu nchini humo kupinga vitendo
vya kikatili vinavyofanywa na jeshi hilo ikiwa ni pamoja na utesaji,
kuwatia raia mbaroni pasipo sababu za msingi na kusema kuwa jeshi hilo
la polisi sasa linaonekana kurejea katika enzi za utawala wa Rais Hosni
Mubarak.
Ukatili
wa aina hiyo wa jeshi la polisi nchini humo ndio uliosababisha
malalamiko yaliyopelekea wananchi wengi wa Misri kushiriki katika
vuguvugu hilo la mwaka 2011.
Rais
El-Sissi alisema lengo la vuguvugu hilo la maandamano ya umma lilipoteza
mwelekeo wake na kuonekana kuwa na mtizamo wa masilahi ya kibinafisi
zaidi kuliko utaifa na kuonekana kuchukua mtizamo wa udugu wa kiisilamu
zaidi ambalo ni kundi lililopigwa marufuku na kuchukuliwa kama kundi la
kigaidi baada ya El- Sissi ambaye ni mwanajeshhi kuongoza harakati
zilizouondoa madarakani utawala wa kundi hilo wa Rais Mohammed Morsi.
Alisema
mapinduzi hayo yalilenga kurejesha heshima na utawala ambao wananchi
wanauhitaji zaidi kwa ajili ya ustawi wa taifa hilo.
El Sissi awataka wananchi walinde Demokrasia
Aliongeza
kuwa Misri ya sasa siyo ile ya jana na kuwa wanajenga taifa ambalo ni
la kisasa zaidi na linalosimamia misingi ya usawa na kidemokrasia na
kusisitiza kuwa demokrasia ya kweli haiji mara moja tu inakuja kwa njia
ya mchakato na kutoa mwito kwa wananchi wa taifa hilo kuilinda kwa
pamoja misingi ya usawa inayojengwa ili kuepuka machafuko yasiyo ya
lazima katika taifa hilo.
Hata
hivyo maelfu ya waungaji mkono wa kundi la udugu wa Kiislamu , pamoja na
watu wengi wenye msimamo wa kati wanaharakati wanaodai demokrasi zaidi
na wengine wamewekwa kizuwizini.
El Sisi
amekuwa akiongoza tangu mwaka 2013 kile ambacho kundi la kutetea haki za
binadamu la Amnesty International linakieleza kuwa ni ukandamizaji
uliopita kiasi dhidi ya wapinzani.
Chanzo:DW
No comments:
Post a Comment