Afisa wa Tume ya Uchaguzi akihesabu kura baada ya kufungwa kwa kituo cha kupigia kura katika mji wa Bangui, Desemba 30, 2015.
Na RFI
Duru ya
kwanza ya uchaguzi wa wabunge nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati umefutwa
Jumatatu hii na Mahakama ya Katiba kutokana na"kasoro mbalimbali".
Mahakama
ya Katiba imethibitisha pambano katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais
kati ya Mawaziri Wakuu wawili wa zamani, Anicet Georges Dologuélé na
Faustin Archange Touadéra.
Chaguzi
hizi mbili, ambazo zinapelekea nchi hii maskini kuondokana na kipindi
cha miaka mitatu ya vita na makabiliano kati ya jamii, zilifanyika
Desemba 30 katika hali ya utulivu wa ajabu. Chaguzi hizi zilishuhudia
kiwango kikubwa cha ushiriki wa wapiga kura licha ya matatizo mbalimbali
ya vifaa.
"Uchaguzi
wa (wabunge) wa Desemba 30, 2015 umefutwa nautarejelewa (...) kwa
sababu ya kasoro nyingi na ushiriki wa wagombea katika kasoro hizo",
Mkuu wa Mahakama ya mpito ya Katiba, Zacharie Ndoumba, amesema wakati wa
mkutano wa hadhara jijini Bangui.
"Baraza
la kitaifa la Mpito la (Serikali, bunge) litaendelea na shughuli zake
mpaka Bunge jipya litakapochaguliwa na kuanza kazi", Zacharie Ndoumba
ameongeza, akinaini kwamba mahakama "imepokea malalamiko 414" kutoka kwa
wagombea waliofanyiwa unyonge.
Uchaguzi
wa wabunge ulifanyika katika majimbo 140 nchini lakini vifaa vya
uchaguzi na kadi nyingi za kupigia kura, vilivyosafirishwa katika dakika
za mwisho, havikufika katika maeneo ya mbali.
No comments:
Post a Comment