Diamond Platnumz amesema akiachana na muziki anataka kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kuweka vitu sawa na kutoa fursa zaidi kwa vijana.
Akizungumza katika kipindi cha Papaso cha TBC FM, Diamond alisema kama akiingia kwenye siasa basi nia yake ni kuwa Waziri wa Michezo.
“Kwa sasa hivi siasa bado ila nikiingia kwenye siasa baadaye akimaliza mheshimiwa Nape nachukua mimi kile cheo cha Waziri wa Michezo,”alisema na kuongeza;
“Kile nakiweza kabisa kwa sababu mimi ukinimbia sijui kuhusu mpira, movie mimi naweza kabisa nikiwa Waziri, nikavifanya na vikawa na maendeleo.
"Ni kitu ambacho naweza siyo nasema nataka kuwa mbunge ila mimi nataka ile siku nimeacha kufanya muziki naingia kwenye siasa basi nakuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na kuboresha vitu”
Diamond ambaye hakuweka wazi kwamba ataingia kwenye siasa kupitia chama gani, mwaka jana katika kampeni za uchaguzi mkuu uliomuingiza rais Magufuli madarakani, alishiriki kikamilifu kwenye kampeni za CCM na kutengeneza wimbo pamoja na video.
No comments:
Post a Comment