Meli ambayo imebebea maelfu ya vitabu, ambayo huhudumu kama maktaba, imetia nanga bandarini Dar es Salaam.
Meli hiyo ina zaidi ya vitabu 5,000 pamoja na video.
Itakuwa bandarini Dar es Salaam kwa muda wa wiki tatu hivi, hadi tarehe 17 Februari
Wananchi wataruhusiwa kuingia kati ya saa tatu unusu asubuhi na saa kumi na mbili jioni Jumanne hadi Jumamosi.
Jumapili, itafunguliwa kati ya saa sita unusu mchana hadi saa kumi na mbili jioni. Jumatatu, haitafunguliwa.
Ada ya
kiingilio ni Sh1,000 za Tanzania.Wanaopanga kuingia, wanatakiwa kupepa
vitambulisho vya kitaifa au pasipoti.Nahodha wa meli hiyo ni Bw Durke.
Wahudumu wote 400 kwenye meli hiyo ni wa kujitolea, hakuna anayelipwa mshahara.
Waziri wa
Elimu Tanzania Joyce Ndalichako, aliyelaki meli hiyo bandarini, amesema
taifa hilo litapanua huduma za maktaba wilayani na vijijini.
Baada ya
kuondoka Dar es Salaam, MV Logos Hope inatarajiwa kuenelea mjini Maputo,
Msumbiji na baadaye Durban nchini Afrika Kusini.
Meli hiyo humilikiwa na shirika lisilo la Kijerumani la GBA (Gute Bucher fur Aller/Vitabu Vizuri kwa Wote
No comments:
Post a Comment