VYAMA VYA SIASA VYAASWA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA ZANZIBAR - LEKULE

Breaking

27 Jan 2016

VYAMA VYA SIASA VYAASWA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA ZANZIBAR

mutungi
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Mhe.Jaji Francis Mutungi ameviasa Vyama vya Siasa kushiriki chaguzi zinazotangazwa na tume za uchaguzi nchini ikiwemo uchaguzi wa Machi 20, mwaka 2016 uliotangzwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).
Kwa mujibu wa barua iliyotolewa kwa vyama hivyo leo na kusainiwa na Jaji Mutungi ilieleza kwamba, kimsingi Sheria ya Vyama Vya Siasa Sura ya 258 inasisitiza vyama vya siasa kushiriki katika chaguzi zote zinazotangazwa na tume za uchaguzi ili kufikia malengo yake ya kushika dola.
“Katika nchi kidemokrasia na kwa chama cha siasa kinachoamini misingi ya kidemorasia ya vyama vingi vya siasa, hakuna njia mbadala kwa chama cha siasa kufikia malengo yake zaidi ya kushiriki uchaguzi.

“Ni wajibu wa kila chama cha siasa nchini kama wakala wa kukuza demokrasia, utawala wa sheria na amani ya nchi, kuwa wa kwanza kutii matamko ya kisheria yanayotolewa na mamlaka husika . Kama kuna chama cha siasa hakiridhiki au kimekwazwa kwa njia moja au nyingine na suala lolote kuhusu masuala ya uchaguzi, njia stahiki na inayonyesha ukomavu wa kisiasa si kuhamasisha kugomea uchaguzi, bali ni vema kikafuata utaratibu uliowekwa katika sheria za uchaguzi,” alisema Jaji Mutungi.

No comments: